Mwandishi Wetu, Mbeya
Angellah Kairuki |
SERIKALI imewaagiza
waajiri wote na watumishi wa umma kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
(TPSC) kwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha fani na taaluma zilizopo
katika sehemu za kazi.
Akizungumza mwishoni
mwa wiki katika mahafali ya 26 ya TPSC Mkoani Tabora, Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora) Angellah Kairuki, al;isema
Chuo hicho kikitumiwa ipasavyo, ufanisi sehemu za kazi utaongezeka.
“Kwa nafasi
yangu kama waziri mwenye dhamana ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana na
viongozi wenzangu, tunaahidi kukijengea chuo uwezo na kukiongezea ufanisi
katika utoaji huduma ya taaluma bora na ujuzi katika maeneo yetu ya
kazi,”alisema.
Alisema serikali
siku zote imejitahidi kuhakikisha kwamba TPSC inatoa kozi ambazo zinatambulika katika mfumo wa
elimu ili wahitimu waweze kukubalika katika soko la ajira badala serikali peke
yake.
“Hatua hii
ilihusisha kuandaa mitaala inayokubalika kitaifa, nakipogeza Chuo Cha Utumishi
wa Umma Tanzania kwa kufanikisha maboresho ya mitaala ya chuo kwa mujinu wa
vigezo vya Baraza la Ithibati la Elimu ya Ufundi (Nacte) na hatimaye
kukiwezesha chuo kupata usajili,”
Waziri
aliwahakikishia wahitimu kwamba vyeti walivyokabidhiwa vinakubalika katika soko
la ajira na pia vinakidhi vigezo vya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa
ngazi ya Stashahada na Shahada.
Naye Mtendaji
Mkuu wa Chuo hicho, Dkt.Henry Mambo alisema Chuo kimeendelea kukua na kuimarika
kwa kuongeza idadi ya wanachuo,vitendea kazi na idadi ya kozi kwa uwiano mzuri.
Alisema hadi
sasa chuo kina kozi zaidi ya 20 katika maeneo ya Menejimenti ya Nyaraka na
Kumbukumbu,Uhazili, Uongozi na Utawala wa Serikali za Mitaa,Rasilimali
Watu,Ununuzi na Ugavi,Sheria na Ukutubi.
Kozi nyingine
ni Menejimenti ya Fedha za Umma na Utawala wa Umma,mafunzo ambayo yanatolewa
kwa ngazi za Cheti na Stashahada.
Alisema chuo
kina matawi sita ambayo ni Dar es Salaam, Tabora,Mtwara,Singida,Tanga na Mbeya.
Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi
4487 walihitimu katika kozi mbalimbali zitolewazo na chuo hicho.Wahitimu ni
Watumishi wa Umma na Watumishi wa Umma watarajiwa.
Dkt.Mambo alisema pia chuo kinatoa ushauri wa
kitaalam katika maeneo ya miundo na mifumo ya utumishi , mpango mkakati ,Mkataba
wa huduma kwa mteja , tathmini na uchambuzi kazi , tathmini ya utoaji huduma
katika utumishi wa umma na usimamizi wa mchakato wa ajira.
Aliyataja baadhi ya majukumu ya Chuo kuwa ni kutoa
mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wa wa umma ili kuwajengea uwezo katika
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
0 comments:
Post a Comment