Butiku: CCM ilishindwa kujikosoa


Suleiman Msuya

Joseph Butiku
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema uamuzi wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuruhusu vyama vingi nchini ulikuja kutokana na kugundua kuwa viongozi na wanachama wengi wa CCM, wameshindwa kujikosoa.

Aidha, Butiku amesema viongozi wanatakiwa kuzingatia miiko mikuu miwili ya uongozi ili kukidhi utumishi uliotukuka na usawa.

Aliyasema hayo katika Kongamano la Kumbukizi ya kuzaliwa kwa Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Butiku aliitaja miiko hiyo kuwa ni viongozi kuamini kuwa binadamu wote ni ndugu na wana haki sawa na kufuata miiko ya Kikatiba, Sheria, kanuni na taratibu.

Alisema haiwezekani mtu akajigamba kuwa anamuenzi Mwalimu Nyerere bila kuzingatia misingi ya udugu, usawa na Katiba kwani ndivyo vitu vilivyozingatiwa na Baba wa Taifa.

Mkurugenzi huyo ambaye pia aliwa msaidizi wa Mwalimu Nyerere, alisema yoyote ambaye ataongoza au kusimamia utumishi bila kufuata hayo atakuwa anajijengea heshima yake binafsi na siyo kwa jamii iliyomchagua.

“Unajua mimi naamini ukipata heshima katika ngazi ya uzee ndio heshima kubwa na hizi zingine za urais si kitu, jambo ambalo najivunia. Naamini viongozi wanatakiwa kuishi katika miiko hiyo ya udugu, usawa na Katiba,” alisema.

Alisema Katiba ndiyo njia na mfumo sahihi wa kushirikisha jamii nzima bila ubaguzi, hivyo kuwataka viongozi kuheshimu hilo na kuachana na dhana ya kufikiria kuwa kila mtu ana mamlaka yake.

Butiku aliyeishia nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM na Serikali alisema katika kuyatimiza hayo ni jukumu la kila mdau kusimamia ukweli kwa kile anachokifanya na kuachana na unafki aliosema haujengi wala kuendeleza Taifa.

Alisema kukiukwa kwa misingi hiyo muhimu kunaweza kusababisha Taifa kufanya kazi yake bila kujadi sheria, hivyo inaweza kuwa sababu ya kuwepo kwa ufa.

Aidha, Butibu aliweka bayana kuwa pamoja na maoni ya asilimia 20 ya Watanzania kutaka uwepo wa vyama vingi, Nyerere alifanya uamuzi wa kuruhusu vyama vingi kutokana na CCM kushindwa kujikosoa.

Butiku alisema CCM ilishindwa kujitathmini, hali ambayo ilitoa ishara ya kupoteza sifa, hivyo Nyerere aliamini kuruhusu vyama vingi kutaweza kufungua kurasa nyingine ya kujitafakari na kujitathmini.

“Ni kweli maoni ya asilimia 20 yalikuwa ni sehemu ya kufanya mabadiliko ila aliona CCM inajisahau na inahitaji kuwa na washindani ili kujitathmini,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo