Salha Mohamed
Kamanda Lucas Mkondya |
NAIBU Kamanda
wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema Jeshi
hilo litawafukuza kazi askari watakaotoa taarifa za raia wanaofichua wezi.
Mkondya alisema
hayo hivi karibuni, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata
malalamiko ya wananchi kwa baadhi ya askari kutoa taarifa za raia wema.
Mkondya
alisema kama kuna askari anayepewa taarifa za uhalifu na kuzitoa atakamatwa,
kufukuzwa kazi na kisha kupelekwa mahakamani.
"Tunampeleka
mahakamani kwa sababu atakuwa amefanya kitendo cha uhaini cha kuhatarisha
maisha ya raia mwema hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi," alisema.
Alisema endapo
mwananchi ataona askari anayetaka kumpa taarifa hamfai basi aende kwa Kamanda
wa Kanda hiyo, Simon Siro.
"Kila
raia aliye na taarifa za raia anayeona huyu matendo yake siyo, atoe taarifa
mara moja ili Polisi ichukue hatua na kumkamata," alisema.
Aliwashukuru
wenyeviti wa serikali za mitaa na viongozi na wananchi kutoa taarifa za
wahalifu hadi mafanikio waliyopata katika kukamata wahalifu.
Mkondya
alisema wananchi wanapaswa kutoa taarifa za watu wa mitaani kwao anayefanya
vitendo vya kutilia shaka watoe taarifa.
Akizungumzia dawa
za kulevya alisema ni lazima Jeshi hilo pamoja na wananchi kupambana kwa hali
na mali kwani matumizi ya dawa hugharimu maisha ya vijana wa Taifa hili.
"Kila
mwananchi kwenye mtaa wake atuletee taarifa na sisi tunamhakikishia
tutazifanyia kazi kwa usiri mkubwa sana," alisema.
Alisema
matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakirudisha nyuma uchumi wa nchi, hivyo ni
muhimu kila mtu akapingana nayo.
Aliwataka
wananchi kushirikiana na Jeshi hilo kutaja wahusika huku akiwahakikishia kutotoa
siri zao.
0 comments:
Post a Comment