HOFU ya maandamano ya Umoja wa
Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) yaliyokuwa yafanyike Alhamisi iliyopita, yamesababisha
baadhi ya watalii waliokuwa wamedhamiria kuja nchini kuangalia kupatwa kwa jua,
kuahirisha safari zao kwa sababu za kiusalama.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Sengeneza Geofrey
alisema alipata taarifa kutoka kwa mwongoza watalii kuwa wageni hao walipata
hofu kuja kuangalia kupatwa kwa jua Septemba mosi.
“Sisi hatufanyi biashara ya
kuongoza watalii, kazi yetu ni kuhimiza watalii waje na kampuni za kupeleka
watalii hao sehemu zao, hao wenye kampuni ndio wanajua,” alisema.
Alisema alipata taarifa kutoka
kwa mwongozaji mmoja watalii kuwa kulikuwa na orodha ya watalii waliotakiwa
kufika kuangalia kupatwa kwa mwezi lakini waliahirisha.
“Kuna kitu kama hicho kweli
kilikuwapo, lakini nilikisikia tulipozungumza na hao waongozaji utalii lakini
kwa idadi ni wengi kiasi gani hatuwezi kufahamu,” alisema.
Alisema mbali na hali hiyo,
lakini walipata watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali huku akibainisha walioahirisha
walikuwa wachache kuliko waliofika kuangalia kupatwa kwa jua.
Alitaja watalii hao ni kutoka
nchi ya Marekani, Uholanzi, Canada, Ujerumani na hata India, huku bara la
Afrika wakitoka Afrika Kusini, Zambia, Malawi, Kenya na wenyeji wa Tanzania
ambapo walikuwapo wakazi kutoka Mwanza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Universal Palagon Links (UPL), mkoani Mbeya, Gabriel Shawa alisema katika
kampuni hiyo kulikuwa na wageni 11 ambao waliahirisha safari ya kufika
kuangalia kupatwa kwa jua Septemba mosi, huku kadhaa wakipeleka tarehe za kuja
nchini mbele.
“Siingiliani sana na kusema kuwa
Ukuta ndio uliosababisha hilo kutokana na tamko la kiusalama kwa upande wao,
labda waliamua kubadili tarehe ya kufika lakini bado biashara kwangu itaendelea,”
alisema.
Alisema anachojali yeye ni kufika
kwa wateja wake ambapo wengine waliahirisha kufika na kudadisi kutokana na
taarifa ya kiusalama ambapo walikuwa na shaka.
“Huwezi kudadisi sana, kwa sababu
nafanya biashara si siasa, 11 waliahirisha kufika lakini siwezi kudadisi sana
kiukuta ingawa idadi hii haijawahi kutokea,” alisema.
0 comments:
Post a Comment