KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, amepokea Tamko la maandishi kutoka kwa muungano wa vyama vya Umoja wa Kiliberari (Liberal International - LI) kuhusu mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar uliotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana na wa Machi 20.
Tamko hilo
limebeba ujumbe wa mwito wa kuheshimiwa kwa haki za binadamu, kurejeshwa kwa demokrasia
na utawala wa kisheria Zanzibar na Tanzania kwa jumla, huku Chama cha Wananchi
(CUF), kikieleza kulipokea kwa mikono miwili kwa imani kuwahaki itatendeka.
Hatua hiyo
ya LI kuandikia UNHRC imekuja wiki kadhaa baada ya Maalim Seif kukutana na
taasisi za kimataifa zinazoshughulikia maendeleo ya demokrasia na utawala bora
na wakuu wa serikali za Marekani, Ulaya na Canada.
Maalim Seif
alifuatana na baadhi ya wasaidizi wake na alifika Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kimaita (ICC) iliyoko The Hague, Uholanzi, ambako aliwasilisha malalamiko
ya uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa Zanzibar kwa alichosema ni idhini ya
viongozi wa CCM.
Kwa mujibu
wa Makamu wa Rais wa LI, Robert Woodthorpe, Ban alipokea tamko hilo na
kuliwasilisha katika kikao cha 33 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa
Mataifa (UNHRC) kinachoendelea New York, Marekani.
Woodthorpe
alinukuliwa na Sauti ya Ujerumani (Deustchewelle) jana akisema suala hilo
liliwasilishwa katika ajenda namba tatu ya UNHRC, iliyokuwa ikijadili mambo
mbalimbali lengo likiwa ni kuitaka Tanzania na Zanzibar kushimu haki za binadamu
na demokrasia.
“Tumeandika
taarifa na tumeiwasilisha kwenye mkutano wa 33 wa UNHRC ambapo LI inataarifu taasisi
za kimataifa, kuongeza msukumo kwa Serikali ya Tanzania kuacha uvunjifu wa haki
za binadamu, kuzuia shughuli za kisiasa na haki zingine kwa wananchi wa Zanzibar,”
alisema.
Alisema
tamko lao limebainisha uwepo wa uvunjifu wa haki za binadamu hasa kwa upande wa
upinzani, ukiwamo ukiukwaji wa demokrasia baada ya uchaguzi wa Oktoba 25.
Woodthorpe
alisema mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif alipeleka taarifa ya
kilichotokea katika uchaguzi huo makao makuu ya IL na baada ya kupitia walijiridhisha
hivyo kupeleka UN.
Alisema
katika tamko hilo wametoa mapendekezo ambayo yanaweza kusaidia Wazanzibari
kujiona sehemu ya watu wenye kuishi katika misingi ya uhuru. Alisema waliiomba
UNHRC kuweka vikwazo vya kisiasa, mali na zuio la kusafiri kwa baadhi ya
viongozi kutokana na ukiukwaji huo wa haki za binadamu na uvunjifu wa demokrasia.
Taasisi
hiyo ambayo CUF ni mwanachama wake, ilitoa mwito kwa wabunge wanaofuata mtazamo
wa kiliberali upande wa serikali na upinzanikatika mataifa yote duniani,
kuchukua msimamo imara kupitia mabunge ya nchi zao na kutoa matamko ya kupinga
walichokiita uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.
Ofisa
Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Alli Kondo
alisema kimsingi hawajapata taarifa rasmi kuhusu suala hilo na kueleza kuwa
wanawasiliana na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ili kupata taarifa.
“Nimewasiliana na idara husika wanasema bado hawajapata taarifa kuhusu suala
hilo, ila wanawasiliana na ubalozi wa Marekani ili kujua nini kinaendelea na
wataeleza,” alisema.
Msemaji wa
CCM, Christopher ole Sendeka alisema chama kilichotajwa kusababisha hali hiyo
kutokea, hakina taarifa yoyote na watatoa taarifa iwapo watahitajika. Sendeka alisema CCM inaamini Uchaguzi Mkuu
Zanzibar ulishamalizika na kwamba yanayosemwa sasa hawawezi kuyazungumzia.
0 comments:
Post a Comment