William Shao |
Uchunguzi
mwingine ulionesha kwamba Waingereza wanapatwa na huzuni na mifadhaiko kuliko
raia wa taifa jingine lolote duniani. Wataalamu wanaamini kuwa mambo hayo mawili
ubinafsi na huzuni yanahusiana.
Utafiti
uliofanywa na Chuo Kikuu cha Northwestern kilichoko Chicago, Marekani,
ulilinganisha jamii mbalimbali duniani, kama zile zinazopatikana katika nchi za
Ulaya na zile za China na Taiwan.
Ilionekana
kwamba kwa kuwa jamii za China na Taiwan zinathamini zaidi ushirikiano katika
jamii badala ya ubinafsi, watu wanalindwa wasipatwe na matatizo ya akili.
Kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na mwanasaikolojia wa Uholanzi, Geert Hofstede,
imegundulika kuwa katika nchi zilizo na jamii zenye watu wabinafsi zaidi,
Uingereza ilishika namba moja katika orodha, ikifuatiwa na Marekani, Australia na
nchi nyingine za Magharibi. Katika nchi za Ulaya, “jamii yenye ubinafsi
inatufanya tuhuzunike,” linaripoti gazeti Telegraph.
Hata hivyo,
kiwango cha huzuni na mfadhaiko katika jamii hizo ni cha juu sana kuliko mahali
pengine popote duniani, kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
uliojulikana kama ‘Depression: A Global Public Health Concern’.
“Tumegundua
uhusiano wa ajabu sana kati ya ubinafsi, huzuni na mfadhaiko,” anasema Dk. Joan
Chiao, mwandishi wa taarifa ya utafiti huo, na kuongeza, “Mataifa yenye watu walio
na ubinafsi zaidi wameonesha kiwango cha juu sana cha huzuni na mfadhaiko.”
“Kiasi cha
mmoja kati ya watu 10 nchini Uingereza anateswa na ama huzuni au mfadhaiko
ikilinganishwa na mmoja kati ya watu 12 katika Bara la Ulaya,” liliandika pia
gazeti la Telegraph na kuongeza:
“Inakadiriwa kuwa kiwango cha mfadhaiko na huzuni nchini China ni kiasi cha
mmoja kati ya watu 25.”
Huenda
wengine wakadhani kuwa ubinafsi huo umechochewa na uzalendo wa Waingereza kwa
nchi yao. Lakini kama ndivyo, kamusi moja inafafanua uzalendo kuwa “kutukuza
taifa moja juu ya mataifa mengine yote na kusisitiza kuendelezwa kwa utamaduni
wake na maslahi ya taifa hilo badala ya mataifa mengine.”
Mtafiti Ivo
Duchacek, ambaye ni profesa wa siasa, alisema katika kitabu chake, Conflict and Cooperation Among Nations: “Uzalendo hugawanya wanadamu katika
visehemu visivyoweza kuvumiliana. Kwa sababu hiyo, watu hujiona kuwa
Wamarekani, Warusi, Wachina, Wamisri, Waperu, au watu wa taifa lingine, kisha
wanajiona kuwa wanadamu ikiwa kwa vyovyote wao hujifikiria hivyo.”
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliandika hivi: “Matatizo mengi tunayokabili
leo ni kwa sababu ya, au yanatokana na mitazamo isiyofaa ambayo tumeisitawisha,
mengine bila kujua. Mawazo hayo yanajumuisha wazo la kwamba ‘nitaitetea nchi
yangu iwe imekosea au la.”
0754/0655-989837
0 comments:
Post a Comment