WATAALAMU wa afya wameshauri kuwa chumvi ni lazima itumike kwa uangalifu ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kumpata mlaji.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Dk. Phili Chilo, alisema chumvi ikitumiwa vibaya
husababisha maradhi ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Alisema wastani wa kiwango cha chumvi unaokubalika kiafya
mtu anatakiwa kula kwa siku nzima ni miligramu 2300 tu, sawa na kijiko kidogo
cha chumvi. Kwa wale wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo na shinikizo la damu
wanatakiwa kutozidisha kiasi cha miligramu 1,500 ya chumvi kwa siku.
Wapo wanaopinga kipimo hicho wanaodai kuwa, watu wanatokwa
sana na jasho, wanaofanya kazi za sulubu, wanamichezo na wanaoishi katika nchi
za joto wanatakiwa kula chumvi zaidi.
0 comments:
Post a Comment