NYAMA ni mojawapo ya mlo unaopendwa na watu wengi. Ukienda kwenye baa, migahawa na hotelini utakuta milo mingi inayoliwa ikiandamana na nyama.
Hii
inatokana na ukweli kwamba wataalamu wa afya wanapendekeza kula mlo kamili,
wakiwa na maana chakula chenye virutubisho vyote, protini, wanga, madini na vitamini.
Vyote hivi wanapendekeza vitumike kwa uwiano sahihi ili kuwa na afya bora.
Protini ni
aina ya viinilishe vinavyopatikana kwa wingi katika nyama. Kazi ya protini ni
kujenga mwili. Nyama ni sehemu ya vyakula ambayo inaonekana kuvuta hamu ya kula
kwa watu wengi. Wanywaji baa hupendelea kula nyama zaidi kama moja ya
kihamasishio cha starehe ya kupata kilevi.
Nyama
inayotumiwa zaidi ni ile inayotokana na ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kuku na kondoo,hata
hivyo inaweza kuchafuliwa na vimelea mbalimbali vya maradhi endapo kanuni bora
za usafi hazitazingatiwa wakati wa uandaaji na utunzaji wa nyama hiyo.
Taarifa ya
utafiti iliyofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) katika maeneo
mbalimbali ya uandaaji wa nyama katika kiwango cha kuwa tayari kuliwa, umebaini
kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa kanuni za afya.
Katika
uchunguzi wao, kanuni hizi zimekuwa zikivunjwa zaidi kwa wale wanaoandaliwa
nyama choma na hizi mara nyingi hufanyika kwenye baa.
Kwa hali halisi
ya mazingira ya Tanzania, watu wengi hupenda kufanya starehe baa ambako hunywa
na kula. Mazingira ya baa nyingi ambazo katika maneo ya mji, unaweza kuziona karibu
kila kona, nyama choma ni moja ya kiburudisho muhimu kinachopatikana kwa wingi.
Kasoro
za utayarishaji
TFDA
inaeleza kuwa kabla ya kuliwa, nyama huweza kuandaliwa kwa njia ya kuchomwa
kwenye jiko la mkaa, kuni, jiko la umeme au gesi hadi hapo inapobadilika rangi
kuashiria kuwa imeiva.
Utayarishaji
wa aina hii hupendwa na walaji wengi kwa kuwa unaamika. Hii ni bala ya kupika
kwa kutumia maji au mafuta yake, hivyo kuwa na ladha nzuri.
Utayarishaji
wa nyama kwa njia ya kuchoma hufanyika kwa wingi kwenye maeneo ya baa, hoteli,
migahawa na hata majumbani.
Hata hivyo,
baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi nyama inayochomwa haiivi vizuri
na hivyo kubaki na vimelea vya maradhi ambavyo ni hatari kwa afya ya mlaji.
Hali hii
inaweza kuwa mbaya zaidi hasa nyama inayochomwa inapokuwa haikukaguliwa na
kupitishwa na mamlaka husika kuwa inafaa kwa matumizi ya binadamu.
Aina ya vimelea
vya maradhi vinavyoweza kupatikana kwenye nyama mbichi ni pamoja na Salmonella,
Compilobacter, Brucella Abortus, L. Monocytogens, C. Bovis, na E. Coli ambavyo
hupatikana kwenye matumbo au minofu ya wanyama husika. Iwapo kanuni za usafi
hazitazingatiwa wakati wa uchinjaji wa mnyama, vimelea hivyo huweza kuingia
kwenye nyama mbichi hasa wakati mnyama anapochunwa ngozi na kutolewa utumbo.
Namna
ya kuchoma nyama
Ili nyama
iweze kuiva vizuri na hivyo kuepuka uchafuzi au uwepo wa vimelea vya maradhi ni
muhimu kuzingatia vigezo kadhaa.
Kigezo cha
kwanza ni ukubwa wa kipande cha nyama ambacho kimewekwa kwenye jiko kwa ajili
ya kuchomwa. Mchomaji anapoweka vipande vikubwa vya nyama inaweza kuiva na kubadilika
rangi sehemu ya nje tu na kuacha ya ndani.
Ili vimelea
vya maradhi viweze kufa, linahitajika joto lisilopungua kiasi cha nyuzi joto 75
hasa kwa sehemu ya katikati ya kipande cha nyama inayochomwa. Kigezo cha pili
ni kiasi cha moto au joto linalotumika kuchomea nyama.
Wachomaji
wengi wa nyama hupenda kuchoma kwenye moto mdogo kwa muda mrefu kwa lengo la
kuepuka nyama isiungue.
Kitaalamu
joto hili linaweza lisiue vimelea vya maradhi bali likawezesha vimelea hivyo
kuendelea kuishi na kuzalisha sumu.
Kigezo cha
tatu ni aina ya vimelea vya maradhi vilivyopo kwenye nyama. Kuna vimelea
ambavyo vina uwezo mkubwa wa kustahimili joto kali. Nyama iliyochafuliwa na
aina hii ya vimelea inahitaji kupikwa kwenye moto mkali usiopungua nyuzi joto 100
ili kuweza kuua viini vya maradhi.
Ili
kupunguza uchafuzi wa vimelea vya maradhi kwenye nyama iliyochomwa, mchomaji
anapaswa kuhakikisha kuwa ananunua ile ambayo na kuruhusiwa kutumiwa na
binadamu. Kanuni hii inalenga kuwatahadharisha wachomaji wa nyama kutonunua nyama
sehemu zisizotambulika ili kuepuka kununua iliyotokana na mnyama mwenye
magonjwa hatari kwa afya ya binadamu.
Eneo la
kuchomea na kuuzia nyama linapaswa kuwa safi na liwe limekaguliwa na kuruhusiwa
kufanyia biashara hiyo na Afisa Afya wa eneo husika.
Maeneo
mengi hususan kwenye minada, nyama inachomwa kwenye mazingira yenye vumbi na
yasiyozingatia kanuni za usafi, hali inayoweza kuhatarisha afya ya walaji.
Vyombo vinavyotumika kukatia na kuuzia pia vinapaswa kuwa katika hali ya usafi
wakati wote.
Wachomaji
wa nyama wanapaswa kuzingatia kanuni bora za usafi na kuepuka mienendo
inayoweza kusababisha uchafuzi wa nyama.
Kwa mfano,
baadhi ya wachomaji nyama hususani maeneo ya baa, hupokea fedha kutoka kwa
wateja na kutoa chenji wakati akiwa anaendelea kutayarisha nyama iliyokwisha
chomwa tayari kwa kuliwa.
Hali hii
inaweza kusababisha nyama ilichomwa kuchafuliwa na vimelea mbalimbali vya
maradhi. Ni vyema mwandaaji wa nyama asijihusishe kabisa na upokeaji wa fedha
wakati anapotoa huduma ya nyama inayochomwa.
Vifaa
vya kuchomea
Vifaa vya
kuchomea nyama vinapaswa kusafishwa kwa maji safi ya moto na sabuni ili
kupunguza idadi ya vimelea ambavyo vinaweza kuwa vimeingia kwenye nyama.
Nyama
inapaswa kukatwa vipande vyembamba kwa ajili ya kuchoma ili sehemu ya katikati
iweze kufikiwa na joto kali lenye uwezo wa kuua vimelea. Ikumbukwe kuwa ili
kuwa na ufanisi katika kuua vimelea vya maradhi ni vizuri mchomaji akaanza
kwanza kwa moto mkali na baadaye mdogo.
Mtayarishaji
wa nyama choma anatakiwa kutenganisha sehemu na vifaa vya kukatia na kuandalia
nyama mbichi na nyama iliyoiva. Uchunguzi unaonesha kuwa waandaaji wengi wa
nyama choma wamekuwa wakitumia meza moja, kibao kimoja na kisu kimoja kwa ajili
ya kukatia nyama mbichi na nyama iliyochomwa.
Hii ni
hatari sana kwa afya ya walaji kwa kuwa upo uwezekano mkubwa wa uchafuzi
kutokea baada ya nyama kuiva.
Nyama
iliyochomwa, kuiva vizuri na kuandaliwa katika mazingira yanayofaa inatakiwa
kuliwa ikiwa bado ya moto. Endapo nyama iliyochomwa itakuwa imepoa, inashauriwa
kurudishwa tena kwenye moto mkali kabla ya kuliwa.
Wachomaji
wengi wa nyama huchukua pande kubwa la nyama na kulichoma na wanapoona limeiva hulitoa
na kulikatakata tena kwa kulipoooza kidogo ili asiungue wakati wa ukataji.
Hii ndiyo
kusema, anaipoozesha ili asiathirike kwa joto kali wakati anaikata na akimaliza
huiweka kwenye chombo tayari kumpelekea mlaji. Matokeo ya mpango wa namna hii,
mlaji hupelekewa nyama ambayo tayari imepoa jambo ambalo ni hatari kwa afya
yake.
Mbaya zaidi
mkataji anaweza akawa anapokea fedha na hata kurejesha chenji, mazingira ambayo
yanamfanya kueneza vimelea vya maradhi kwa nyama anayopelekewa mteja.
0 comments:
Post a Comment