Lissu ashinda kortini kusubiri wateja



MWANASHERIA Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, jana al­itinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuangalia kama watuhumiwa walioshikiliwa na Polisi kwa kesi za uchochezi wamefikishwa ku­somewa mashitaka yao au la.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya chama hicho kupitia kwake kueleza kuwa kuna watu 10 wamekamatwa kwenye vituo vya Polisi huku 73 wakiwa taar­ifa zao hazikukamilika kutokana na kudaiwa kuandika taarifa za kichochezi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Serikali iliyoko madarakani na kuvaa fulana zi­lizoandikwa ‘Tupinge Udikteta Uchwara’ jambo ambalo ni uki­ukwaji wa sheria.

Kutokana na hali hiyo Lissu alisema kama watu hao ha­wataachiwa leo (jana), wale 10 ambao wanafahamika watakuwa hawajapelekwa mahakamani au kuachiwa kwa dhamana ya Polisi, chama hicho kitakwenda Ma­hakama Kuu kufungua maombi kwa mujibu wa utaratibu wa she­ria unaoitwa ‘Habeas Corpus’.

Alisema mawakili hao watala­zimika kutumia sheria hiyo, ili Mahakama itumie mamlaka yake ya kuiagiza mamlaka yoyote ya kiserikali, akisema kifungu cha 390 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, kinaruhusu Mahakama Kuu kutoa amri ya kuelekeza mtu anayeshikiliwa kinyume cha sheria, kuletwa ma­hakamani au kuachwa huru.

Akizungumza na JAMBO LEO akiwa mahakamani hapo jana, Lissu alisema lengo la kwenda hapo lilikuwa ni kuangalia kama watuhumiwa hao wamefikish­wa na baada ya hapo azunguke mikoa mingine.

Hata hivyo, Lissu alisema baada ya tamko lile, watu 10 ambao walipelekwa katika kituo kikuu cha Polisi na cha Oysterbay wal­isharudishwa kwenye maeneo yao ili kupelekwa mahakamani.

“Kuna wale watu 10 walioku­wa wamekamatwa katika vi­tuo hivyo, waliachwa siku ile ile ambapo wengine walirudishwa Morogoro, Dodoma na taarifa zilizopo ni kuwa walipelekwa mahakamani leo (jana), na mimi nipo hapa Kisutu kuangalia kama wa Dar es Salaam wataletwa,” alisema Lissu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Lissu alisema lengo lake ni ku­wataka Mkuu wa Polisi nchini, makamanda wa mikoa na polisi wengine nchini, kueleza Ma­hakama ni kwa nini wameshikil­ia watu hao, kwa nini wanawatesa Mikocheni, kwa nini wanawapa adhabu za kinyama na kwamba wameshaandaa hati za kupeleka mahakamani ili viongozi hao wakubwa wa Polisi waeleze.

“Tunataka viongozi hao wase­me ni lini Katiba iliruhusu wa­fanye hivyo, maana kwa mujibu wa sheria ya magazeti ambayo imetushitaki, kifungu cha 32, inaeleza kuwa halitakuwa kosa kutoa kauli ambazo lengo lake ni kuonesha Serikali imekosea na hatujafanya kosa la jinai, hivyo waliokamatwa kwa kosa hilo ha­wana kosa,” alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu jana jioni, Lissu alisema hatimaye washitakiwa wake watano wali­fikishwa mahakamani hapo, lak­ini hawakupandishwa kizimbani kwa kuwa waendesha mashitaka hawakuwa na hati za mashitaka.

Kutokana na hali hiyo alisema waliamriwa kurudi mahakamani hapo leo, akalaumu Polisi kwa kukaa na watuhumiwa siku 20 na kuwapeleka mahakamani bila hati hizo na kusema ni uzembe.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo