RAIS John Magufuli amemwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa
jana kwa vyombo vya habari kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uapishaji huo
ulifanyika jana.
Taarifa hiyo ilisema Balozi Dk
Dau (pichani) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi Dk Aziz
Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki na Kikanda.
Wakati huo huo, Rais Magufuli
aliwaapisha makatibu tawala wa mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Walioapishwa ni Eliya Ntandu
anayekuwa Katibu Tawala wa wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Februari, Adoh
Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Mapunda anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Benedict ole Kuyan ambaye amestaafu, Tixon Nzunda anakuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies
Pangisa ambaye amestaafu.
Baada ya kuapishwa, Balozi Dau na
makatibu tawala hao watatu walikula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi
wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda na
kushuhudiwa na Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment