Salha Mohamed
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili (MNH), imewasimamisha kazi wafanyakazi 31 baada y kubainika wakitumia vyeti bandia huku wengine
48 wakitiliwa shaka uhalali wa vyeti vyao.
Tayari
watumishi hao wameondolewa kwenye mfumo wa kumbukumbu za kiutumishi na mishahara,
baada ya uhakiki huo kukamilika.
Uhakiki huo
unaofanywa na Baraza la Taifa la Mitihani (NACTE) umekuja ikiwa ni utekelezaji
wa agizo la Serikali kutambua na kuondoa watumishi hewa na wasiokuwa na sifa kwenye
nafasi mbalimbali nchini.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MNH, Aminiel Aligaesha alisema wafanyakazi
waliosimamishwa, 11 ni wauguzi, watatu wahudumu wa afya, wahasibu wawili,
watunza kumbukumbu za afya ya wagonjwa watano, makatibu muhtasi wawili,
wafanyakazi wa maabara watatu, mfamasia, karani wa masjala, fundimchundo, dobi
na Ofisa Ustawi wa Jamii.
“Muhimbili
inaendelea na uhakiki wa vyeti vya wafanyakazi kupitia NECTA ambapo hadi sasa
tayari wafanyakazi 1,600 wamehakikiwa vyeti vya kidato cha nne kati ya
wafanyakazi 3,000 waliopo,” alisema.
Alisema
katika mchakato wa uhakiki wa wafanyakazi hospitalini hapo bado wafanyakazi
1,400 hawajahakikiwa na kwamba wanaendelea kuhakikiwa. Alisema watumishi
waliosimamishwa wamewaandikia barua za kujieleza kila mmoja ndani ya siku 14
kwa mujibu wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma, ili kuwapa nafasi ya kujitetea
kabla ya hatua stahiki.
“Tumebaini
kuwa wafanyakazi 48 vyeti vyao vinatia shaka uhalali wao hivyo tumewaandikia barua
ili kuleta vyeti halisi ili kuchunguzwa zaidi na Mamlaka husika,” alisema.
Alisema
kati ya 48 wafanyakazi 23 ndiyo walioleta vyeti na ambavyo tumevipeleka NACTE ambapo
sasa wanasubiri waliobaki 25 wapeleke.
0 comments:
Post a Comment