Kwa mujibu wa Sheikh Jalala, picha hiyo imesambaa kwenye mitandao
ya kijamii ikionesha nguruwe akiwa amekaa juu ya nyumba takatifu ya Makka
(Al-kaaba) na kuielezea hali hiyo kwamba ni hatari na udhalilishaji.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Sheihk Jalala
alisema ni muhimu TCRA imchukulie hatua stahiki kama walivyochukuliwa hatua
watu wengine waliofanya makosa katika masuala ya mitandao.
“TCRA ni wajibu wao kuangalia mambo yaliyokwenda kinyume katika
mitandao ya kijamii, wachukue hatua za haraka, kwasababu tumeona matukio madogo
tu yaliyotokea mamlaka imechukua hatua za haraka,”alisema.
Alisema udhalilishaji huo ni tukio kubwa na mamlaka hiyo
haipaswi kulinyamanzia suala hilo, huku huku akivitaka vyombo vya usalama
kutambua kwamba matukio kama hayo yanaweza kuenea na kuvunja heshima ya vitu
vinavyoheshimiwa na kusababisha mvutano.
Alisema ni vema mamlaka ikaliangalia hilo kwa jicho la
pekee ili tukio hilo lisihatarishe maisha. “Al-Kaaba ni nyumba takatifu sana
kwa Waislam, Al-Kaaba ni Qibla ya Waislam, Al-Kaaba kwa itikadi ya Kiislam ni
nyumba ya Allah, Al-Kaaba kwa Itikadi ya Kiislam ndio nyumba ya kwanza
iliyojengwa kwa ajili ya kumuabudu Allah; ni mahala patakatifu mno,” alisema.
Alisema aliyechora picha hiyo amefanya utovu wa nidhamu
na kwamba ni hatari kwani si jambo jema kushambulia kitu kitakatifu kwa dini
nyingine.
Alisema jambo linalofanana na hilo linaweza yanaweza
kuamsha hisia za watu ambao utakuwa hatari kwa watanzania na kwa taifa, ambapo
tayari kiongozi huyo akitambua yakwamba kuna sheria za mitandao.
“Tunatoa wito kwa TCRA kwamba kulinyamazia tukio hili ni
kusababisha kuvunja utulivu na amani tuliyokuwa nayo katika ardhi ya Tanzania,
sote tunatambua ya kwamba hakuna mivutano hatari na vita hatari na migongano
hatari kama migongano ya wanadini,”alisema.
0 comments:
Post a Comment