Pia imeunga mkono uamuzi wa kuwasimamisha uanachama viongozi
hao na aliyekuwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Jidawi
Chande, alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam ambapo alisema
uamuzi huo una lengo la kukifanya chama kizidi kuendelea.
“Sisi kama jumuiya ya vyuo vikuu wa CUF tawi la Mlimani
tunakubaliana na kupongeza uamuzi wa Baraza Kuu na tunaziomba mamlaka zingine
ndani ya chama ziendelee kufanya uamuzi mgumu wa kujenga chama chetu pale inapobidi,”
alisema Chande.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa Jumuiya hiyo inalaani fujo
na kauli za kibaguzi zinazoendelea kutolewa na Profesa Lipumba na baadhi ya
wafuasi wake kama ile ya Sakaya kuwa chama kina mpasuko wa Bara na Visiwani
kama alivyonukuliwa na magazeti nchini.
“Ikumbukwe, kuwa Profesa Lipumba alikuwa Mwenyekiti wa Cuf
kwa mujibu wa Katiba ibara ya 91 (1) na kwa kuheshimu na kutambua umuhimu wa
Katiba pia Profesa Lipumba alitumia Katiba ya chama ibara ya 117 (1) inayompa
uhuru kiongozi kujiuzulu wadhifa wake na alifanya hivyo kama Katiba inavyoelekeza.
“Pia ibara ya 117 (2) inaelekeza kiongozi atakayejiuzulu
lazima barua yake ipelekwe kwenye mamlaka iliyomteua au kumchagua ili kukubali
au kukataa kujiuzulu kwake, na ndivyo ilivyokuwa kwenye mkutano mkuu wa Agosti
21 na kukubali kujiuzulu kwake, hivyo basi kutokana na hayo ni wazi fujo na
vurugu zinazofanywa na Profesa Lipumba hazina nia njema na Cuf bali ku-gawa
chama,” alisema.
Alisema wao wanazuoni wanamshauri Profesa Lipumba
kuachana na mpango wake wa kuvuruga chama kwa kuwa anachofanya anajidhalilisha
na kujishushia heshima aliyojijengea miaka mingi katika jamii ndani na nje ya
nchi.
0 comments:
Post a Comment