Abraham Ntambara
BARAZA la
Vijana wa Chadema (BAVICHA) limempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza
ahadi yake ya kununua ndege wakisema kwa teknolojia ya leo ingekuwa vyema kama
angenunua ndege kubwa kuliko Bombardier Q400.
Akizungumza
na JAMBO LEO jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Julius Mwita
alimpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake hiyo.
“Kwanza
nimpongeze Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake, kwani kuna viongozi wengine
wemekuwa wakiahidi bila kutekeleza,” alisema Mwita.
Lakini
pamoja na kupongeza, Mwita alisema kwa maendeleo ya kiteknolojia ya leo si vema
kujivunia kwa kununua ndege hizo, kwa kuwa badala ya kusonga mbele “ni kama
tumerudi nyuma kwa takribani miaka 50”.
Alisema ili
kuendana na wakati huu wa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, zingenunuliwa
Airbus A310 au 308 za kubeba abiria wengi ili kusaidia kwenye ushindani mkubwa
wa kibiashara na mashirika mengine.
Aidha,
alisema itakuwa vigumu kwa watu wenye haraka kutumia ndege hizo akitolea mfano
kwamba zikitumika kwa safari ya Dar es Salaam - Mwanza ni saa 3:45 wakati Airbus
inatumia saa 3:20.
Mwita
aliongeza kuwa ndege hizo hazikidhi mahitaji kwa kuwa ni chache wakati nchi ni
kubwa ambapo wahitaji wa usafiri huo ni wengi hivyo kwa msingi huo angesubirikununua
angalau nne ili kuleta alichokiita maana zaidi kuliko sasa. Hata hivyo,
akizindua ndege hizo jana, Rais Magufuli alisema Serikali itanunua ndege kubwa
mbili siku za karibuni, moja ikibeba abiria 160 na nyingine 240.
0 comments:
Post a Comment