Alisema moja ya malengo katika ilani ya CCM ni kuhakikisha kila
mtoto nchini anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.
“Nafahamu shirika lenu la Room to Read limekuwa likitumia mbinu
mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa kujenga maabara katika shule zetu,
kutoa vitabu na mambo mbalimbali katika kupambana na elimu,” alisema.
Alisema takwimu za kitaifa za Sensa ya Makazi na Watu ya mwaka 2012
zinaoonesha asilimia 22 ya Watanzania haiwezi kusoma na kuandika kwa ufasaha.
Takwimu hizo zilionesha pia asilimia 81.7 wana elimu ya msingi na
asilimia 14.4 elimu ya sekondari na asilimia 2.3 elimu ya chuo.
“Kwa mfumo unaofanywa na Room to Read katika kuhakikisha wanafunzi
wanajua kusoma na kuandika wafikapo darasa la tatu ... tunapaswa kujifunza ili
kuhakikisha ifikapo 2030 tunakuwa tumefanikiwa,” alisema.
Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inasema ‘Kuandika
Yaliyopita, Kusoma Yajayo’ itumike kutafakari kufuta ujinga.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter
Mwakambwale alisema siku ya usomaji duniani ni muhimu kwa wadau wa elimu
wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio ya kiserikali na
serikali.
Alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Septemba 9, ikiwa
ni kutimiza Azimio la Tehran lililopitishwa mwaka 1965 ambapo kwamwaka huu
wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1966.
“Kutokana na kuwepo kwa mitihani ya taifa ya darasa la saba, sisi
Room to Read na washiriki wenzetu tuliona ni vema kuadhimisha siku hiyo ili
kupisha tukio muhimu la wadau wetu,” alisema.
Mwakambwale alisema takwimu za Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka 2015 zinaonesha hali ya usomaji
duniani katika nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ni ya
pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha Watanzania wanaojua kusoma, kuandika na
kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.
Alisema Burundi inaongoza katika nchi za ukanda huo kwa asilimia
85.6 ya wananchi wake kujua kusoma na kuandika.
0 comments:
Post a Comment