DK. STEPHEN KISAKA |
KAMA tulivyoona katika sehemu iliyopita kuwa picha, harufu
au sauti huhusika kwa kiasi kikubwa katika kuamsha nguvu za kiume, pia tunaona
lipo jambo jingine ambalo huhusika pia katika kuamsha nguvu za kiume.
Hisia: Katika eneo hili hisia
kupitia katika mguso wa sehemu ya mbele
ya uume au hisia kupitia kuchochewa kwa mishipa ya fahamu kupitia kujaa kwa
kibofu cha mkojo. Hali hizi mbili huamsha chocheo ambalo hupeleka taarifa haraka
katika mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo na ghafla uamko hutokea.
Na hili limethibitishwa na watafiti wengi kwani ni mara
nyingi wakati wa asubuhi uume huwa unakuwa umesimama kwa walio wengi na hata
kwa watoto wadogo nyakati hizi za asubuhi na punde hukojoa.
Tatizo la kimwili: Ili uweze kuwa
na nguvu imara za kiume ni lazima uwe na mfumo mzuri wa mzunguko wa damu katika
mwili wako, kama una matatizo ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa midogo au
magonjwa kama ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari na
mataizo ya tezi la shingo.
Matatizo mengine mfano magonjwa ya mishipa ya fahamu,
upasuaji kipindi cha nyuma, matatizo ya uti wa mgongo, matatizo ya tezi dume
pia nayo yametajwa kuhusika na tatizo hili.
Tatizo la kiakili jamii: Hapa
tunaona matatizo kama msongo wa mawazo, matatizo ya kiuhusiano
(mume na mke au mtu na mpenzi wake), matatizo ya ajira, ya kifedha, ukichaa au
uwendawazimu. Matatizo mengine yanasababishwa na uvutaji sigara, unywaji wa pombe,
ukosefu wa usingizi wa kutosha na utumiaji holela wa dawa.
Msongo wa mawazo na hofu: Msongo wa
mawazo na woga au hofu pia vimeonekana kuwa ni tatizo kubwa katika suala zima la
upungufu wa nguvu za kiume au kushindwa kuwa na nguvu za kiume (hasa msongo wa
mawazo unapokuwa katika suala zima la ndani ya kifamilia au suala la kifedha)
Tunaweza kusema kuwa ili kuweza kupata suluhisho la
kudumu daktari au muuguzi anayekutana na mgonjwa wa namna hii ni lazima aweze
kubaini tatizo na kutafuta mbinu za kiushauri nasihi ili kuweza kupata suluhisho.
Kama tatizo la upungufu wa nguvu za kiume litakuwa
limeingia au kuangukia katika makundi mawili yaani mgonjwa kuwa na tatizo
physical na tatizo psychological basi tatizo hili huenda likawa gumu zaidi
tofauti na likiwa katika kundi moja.
Tunashauri wale wote wenye tatizo hili waende hospitali
mapema kuonana na wataalam na kuwaeleze matatizo bila kuficha ili daktari aweze
kuwasaidia na hivyo kupata suluhisho la kudumu la tatizo husika.
Kinga: Mwanaume anaweza kujikinga na
tatizo hilo kuwa na afya nzuri, kula lishe kamilifu, kupunguza uzito kwa mwenye
uzito mkubwa, kuacha kuvuta sigara, kufanya mazoezi mara kwa mara, kuacha pombe
au utumiaji wa dawa za kulevya, kuacha utumiaji wa dawa kiholela (dawa za
kujinunulia ovyo ovyo).
Pia kuhakikisha unapata tiba haraka kwa anayesumbuliwa
magonjwa mbalimbali yakiwemo moyo na sukari.
Matibabu: Matibabu kulingana na tatizo
lako yapo endapo utafika hospitali mapema. Ni hatari kuamua kujinunulia dawa
madukani au mitaani na kumeza kabla ya uchunguzi wa tatizo lako kwani unaweza
kupata tatizo lakini halihitaji vidonge pekee.
Uchunguzi wa kina na ushauri stahiki na mahusiano mazuri
kati yako na daktari wako pamoja na kufuata kanuni zote za afya ndiyo njia bora
na pekee ya kuweza kupata suluhisho lako.
Kama tatizo lako ni msongo wa mawazo utokanao na ajira au
mambo ya kifedha jiunge na vikundi vidogovidogo vya ujasiriamali katika
kuanzisha biashara au kujiajiri ili kuweza kujikwamua katika hali ya kiuchumi.
Maoni au maswali tuma kwa simu 0713247889
au kwa baruapepe: afya@jamboleo.net
0 comments:
Post a Comment