Wakurugenzi walioteuliwa na Magufuli ‘wapotea’


KUMETOKEA sintofahamu kuhusu wapi waliko wakurugenzi 12 kati ya 185 walioteuliwa na Rais John Magufuli.

Hali hiyo inachangiwa na uteuzi wa wakurugenzi wapya wa hal­mashauri, miji na manispaa ikiwa ni miezi miwili tu tangu uteuzi wa awali.

Hivi karibuni, Rais Magufuli ali­teua wakurugenzi wapya 13, mmoja akijulikana kuwa anaziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mku­rugenzi wa Halmashauri ya Baga­moyo, Azimina Mbilinyi.

Kulingana na uchunguzi wa JAM­BO LEO, hakuna taarifa ambayo iliwahi kutolewa na Serikali kupi­tia ofisi yoyote, kuhusu mabadiliko hayo, tofauti na Mbilinyi ambaye Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilitoa taarifa kuwa uteuzi wake umetenguliwa.

Kwa wakurugenzi wengine aki­wamo wa Manispaa ya Dodoma, Dk Leonard Masale ambaye nafasi yake imechukuliwa na Godwin Ku­nambi, hakuna taarifa za wapi ali­pangiwa baada ya uteuzi wa awali.

Katika Halmashauri ya Tarime, Mkurugenzi wa awali alikuwa Apoo Tindwa na sasa ni Elias Ntiruhun­gwa, Bukoba nafasi ya Makonda Ste­phen ilichukuliwa na Mwantumu Dau na Ukerewe ya Tumaini Shija imechukuliwa na Frank Bahati.

Katika Halmashauri ya Mbulu, awali alikuwapo Festi Fwema na nafasi yake kuchukuliwa na Hud­son Kamoga, Nsimbo ilikuwa ya Joachim Nchunda lakini kwa sasa ni ya Mwailwa Pangani, Nkalama ali­kuwapo Martin Mtanda lakini sasa amekwenda Godfrey Sanga.

Aidha, hali kama hiyo ilitokea ka­tika Halmashauri ya Ulanga ambako Mkurugenzi aliyekuwapo kwa mu­jibu wa uteuzi wa awali, ni Audax Rukonge na mpya sasa ni Yusufu Semuguruka.

Nachingwea, Mkurugenzi alikuwa Bakari Mohamed Bakari na sasa ni Bakari Mohamed, Kibondo alikuwa Shelembi Manolo na nafasi yake ku­chukuliwa na Juma Mnweke, Man­ispaa ya Moshi alikuwapo Michael Mwandezi na sasa yupo Butamo Ndalahwa huku Karatu ilikuwa ya Banda Sonoko lakini sasa ni Waziri Mourice.

Alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ta­wala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Musa Iyombe alisema wateule wapya walikuwa wanaziba nafasi zilizokuwa wazi, kwa kuwa wateule wa awali walishindwa kuki­dhi baadhi ya vigezo kama afya, ud­huru na vingine.

“Walioteuliwa wanajaza nafasi badala ya wa awali kushindwa kuki­dhi baadhi ya vigezo vikiwamo vya afya, udhuru na vingine,” alisema.

Sababu hizo za Iyombe zinatia sha­ka kama wateule hufanyiwa uchun­guzi kabla ya kupewa nafasi huzo na au kama huulizwa kabla.

Kwa kipindi cha miezi 10 ya uon­gozi wa Rais Magufuli ameondoa wateule wake wapya zaidi ya watano ambapo alianza na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilan­go-Malecela kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu wafanyakazi hewa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kwa kulewa bungeni, Mkuu wa Wilaya ya Ikun­gi , Emil Ntakamulenga ambaye alitumbuliwa siku ya kiapo Ikulu na Mbilinyi.

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo