KUNDI la wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jana lilijikuta katika hali ya sintofahamu, baada ya kuzuiwa kuingia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kushuhudia kuwasili kwa ndege mpya aina ya Bombadier Q400 Next- Gen, ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Awali,
wananchi walitakiwa kujitokeza kushuhudia ndege hiyo ikiwasili, lakini baadaye
taarifa zilieleza kuwa hafla ya mapokezi yandege hiyo zimefutwa na isingewasili
jana kama ilivyotangazwa.
Waandishi
hao waliwasili JNIA tangu saa tano asubuhi kwa ajili ya mapokezi hayo, lakini hawakupata
ushirikiano kutoka kwa maofisa wa Wizara ya Uchukuzi na Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege (TAA), ambao walitupiana mpira wa kuhusika kutoa taarifa sahihi na ruhusa
ya kwenda kushuhudia kuwasili
kwa ndege
hiyo.
Miongoni
mwa vyombo vya habari vilivyokumbwa na adha hiyo mbali na gazeti hili ni BBC,
ITV, Azam TV, Chanel Ten, Ayo TV, ZBC, TBC, Mwananchi, JAMBO LEO, Mtanzania na
Radio France (RFA).
Hadi
waandishi wetu wanaondoka uwanja wa ndege wa zamani (Terminal I) saa nane
mchana, hawakufanikiwa kuingia uwanjani kushuhudia ndege hiyo.
Yawasili
Hata hivyo,
baadaye Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa alitoa taarifa
kwa vyombo vya habari za kuwasili kwa ndege hiyo mpya ya kwanza iliyonunuliwa
na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na ATCL, iliyotua jijini ikitokea Canada
ilikotengenezwa.
Kwa mujibu
wa Msigwa, ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua saa 6:15 mchana, kisha
kupewa heshima maalumu, ambayo hutolewa kwa ndege mpya inayotua nchini mwake.
0 comments:
Post a Comment