Rais John Magufuli |
Aidha, wametoa angalizo kwa Serikali kuhusu taarifa za
kutaka kukifuta chama hicho, wakisema uamuzi huo utahatarisha amani ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Baraza hilo,
Roderick Lutembeka alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, siku
saba baada ya Chadema kuahirisha maandamano na mikutano ya kupinga wanachamini
ni ukiukwaji wa demokrasia nchini.
Chadema kupitia Kamati Kuu yake ya Agosti 27 walitangaza
mkakati mpya wa kudai demokrasia ambao ulipewa jina la Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (Ukuta), ambao ulisababisha taharuki nchini kwa kilichohofiwa
kuwa ni uvunjifu wa amani.
Lutembeka alisema uamuzi wa viongozi hao wa dini
kuingilia kati mgogoro huo na kuomba Chadema isubiri kabla ya kuchukua hatua,
ulikuwa wa busara hivyo kumwomba Rais Magufuli awapokee na kuwasikiliza.
Alisema viongozi wa dini ni muhimu katika jamii iwapo
Rais atashindwa kuwasikiliza, atadhihirisha kwa jamii kuwa ni jeuri na mwenye
kiburi.
Alisema uamuzi wa viongozi na Kamati Kuu kuahirisha maandamano
na mikutano ni ishara tosha kuwa chama hicho ni cha kidemokrasia na haki, kwa
kuonesha usikivu na uvumilivu.
Lutembeka alisema wanatumia nafasi hiyo kupongeza wadau
walioshiriki kuepusha mgogoro ambao ungetokea kwani ishara zilionesha kuwa
Serikali na Jeshi la Polisi walijipanga kuleta machafuko nchini.
Kuhusu mpango wa kufuta chama hicho, Katibu huyo alisema
katika uchunguzi wao, walipata taarifa zinazopangwa na Serikali kwa kushirikiana
na Ofisi ya Msajili wa Vyama ili kuifuta Chadema.
Alisema iwapo Serikali itafikia uamuzi huo ni dhahiri
inataka kuhatarisha amani na upendo uliopo nchini kwani hawatakuwa tayari
kukubaliana nayo.
“Wakati kukiwa na jitihada za kurejesha uhusiano mzuri
baina ya pande ambazo zinakinzana kwa mujibu wa Sheria na Katiba tumepata
taarifa kuwa upo mkakati wa kufuta chama, kwa hili hatutakubali,” alisema.
0 comments:
Post a Comment