BAADA ya Mahakama ya Rufaa kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, wake wa marehemu hao wamesema wanajipanga kulishtaki Jeshi la Polisi ili liwalipe fidia.
Mahakama ya
Rufani ilitoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa Christopher Bageni Septemba 16,
baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya wafanyabiashara hao watatu wa madini;
Mathias Lunkombe, Sabinus Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi na ndugu yake
Ephrahim Chigumbi na dereva teksi Juma Ndugu. Mauaji hayo yalifanyika katika
Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.
Katika
hukumu hiyo iliyotolewa na jopo la majaji watatu; Benard Luanda, Sauda Mjasiri
na Semistocles Kaijage, aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam
(RCO), Abdallah Zombe na wenzake wawili walinusurika baada ya upande wa mashitaka
kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao.
Pamoja na
Zombe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao waliachiwa huru ni ASP Ahmed Makelle
na Koplo Rajabu. Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo, Januari 14, 2006.
Msimamo
wa wajane Wakizungumza kwa
nyakati tofauti, wake wa marehemu walisema hawajaridhishwa na hukumu hiyo kwa kuwa imemtia hatiani mtuhumiwa mmoja tu.
Hata hivyo,
walisema ilimradi imethibitika kwamba Polisi waliua, wanajipanga kufungua kesi
ya madai ili walipwe fidia, wakieleza kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona
Serikali imezitelekeza familia za marehemu hao kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Mke wa
marehemu Mathias Lunkombe aliyeachwa na watoto wawili, Mapha Kazingoma alisema
hali ya maisha baada ya kifo cha mumewe ilikuwa mbaya kutokana na kulazimika
kulipia kodi ya nyumba na gharama za shule kwa watoto.
Mjane huyo
alisema kwa kuwa tayari Serikali kupitia mahakama imejiridhisha kuwa wanaume
zao waliuawa kimakosa, kuna haja ya kudai fidia ili kupunguza uchungu waliopata
na makali ya maisha.
“Tuko
katika mchakato wa kukutana wote (wake wa marehemu) ili tuone tunafanyaje
kufungua kesi hiyo, lakini lazima tulipwe fidia kwa kuwa sasa imethibitika kuwa
waume zetu waliuawa kwa makusudi,” alisema.
Mjane huyo
alimwomba Rais John Magufuli kuzisaidia familia za marehemu hao ili zipate haki
waliyokuwa wakiisotea siku nyingi. Aliyekuwa mke wa marehemu Sabinus Chigumbi
maarufu kwa jina la Jongo, Theresia Maswanyiaalisema kuwa kitendo cha kutelekezwa
na Serikali kimeendelea kusababisha majonzi kwao, kwani licha ya kuwa na
majukumu ya malezi ya watoto watano alioachiwa na marehemu mumewe, hakuna
msaada wowote anaopata kutoka serikalini.
Theresia
ambaye kwa sasa anaendesha maisha kwa kutegemea kodi ya nyumba aliyoachiwa na
marehemu mumewe, alisema mara baada ya hukumu hiyo kutolewa wote wamekutana na
kuweka mikakati ya kufungua kesi ya madai ili Serikali iwalipe fidia. “Kwa kweli
suala hilo kwetu halijaisha, tunakusanya nguvu ili tufungue madai watulipe
fidia,” alisema mjane huyo.
Polisi
wasimulia marehemu walivyouawa Katika
hatua nyingine, baadhi ya
askari polisi wamesimulia
tukio la mauaji ya wafanyabiashara hao wa madini wakieleza kuwa lilikuwa ni ukatili wa kutisha. Polisi
hao waliokuwepo mahakamani
siku ya hukumu walisema
kulichofanyika
ni unyama wa kutisha,
hivyo hukumu iliyotolewa ni sahihi.
Huku
wakiomba wasitajwe gazetini, polisi hao walisema kabla ya kuuawa,
wafanyabiashara hao waliomba askari hao wasimuue mmoja kati yao kwa sababu
alikuwa bado mwanafunzi na kwamba hata kiumri alikuwa mdogo.
“Waliomba
aachwe ili aje alee famili zao, kwa sababu wao walikuwa tayari kufa kwa sababu tayari
walishaelezwa kuwa watauawa,” alisimulia askari huyo. “Licha ya maombi hayo,
yule waliyeomba aachwe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuuawa kwa kupigwa risasi na
baada ya tukio hilo, ndugu wa mwanafunzi huyo ambaye alikuwa miongoni mwa
walioomba alilamba damu ya ndugu yake.”
Alifafanua:
“Baada ya kulamba damu hiyo huku akiwa amepiga magoti kama walivyokuwa
wameelekezwa, alilala chini tayari kwa kumiminiwa risasi ndipo naye aliuawa kwa
kumiminiwa risasi kwa nyuma.”
Askari
mwingine alisema damu ya wafanyabiashara hao na dereva teksi itaendelea
kuwatafuna hata wale ambao hawakupatikana na hatia kwa mauaji ya vijana hao.
“Mimi ni
askari lakini naamini vijana hao hawakuwa na hatia, damu yao itaendelea kuwatafuna
wote, hata walioachiwa huru kwenye kesi hiyo kwani hakuwa Bageni peke yake na
kilichofanyika ni ukatili wa wazi,” alisema..
0 comments:
Post a Comment