Maandamano yanachangia kutatua matatizo?


Wananchi wakiandamana
William Shao

Maandamano mengi yanachochewa na mambo kadhaa. Moja ni kutoridhishwa na mifumo ya kijamii. Kwa kawaida, kama matokeo ya utafiri mmoja wa Brazil unavyosema, watu hawana tamaa ya kuandamana wanapoona kwamba serikali na hali ya uchumi inatimiza mahitaji yao.

Wao hupeleka matatizo yao kwa wenye mamlaka. Kwa upande mwingine, watu wanapoona wenye mamlaka ni wafisadi, hawafuati haki, na wanawapendeleatuwatuwachache, basiwao huasi.

Jambo jingine linalosababisha maandamano ni kichocheo. Mara nyingi, tukio fulani huwasukuma watu watende, waache kufikiri kwamba hawawezi kufanya lolote na kuanza kuamini kwamba lazima wachukue hatua fulani.

Gazeti ‘The Times of India’ liliandika kuwa mgomo wa kususia chakula ulioanzishwa na mwanaharakati Anna Hazare ili kupinga ufisadi ulisababisha maandamano yaliyofanywa na wafuasi wake katika miji 450.

Duniani kote, ufisadi na dhuluma imeenea sana leo kuliko wakati huo. Sasa kuliko wakati mwingine wowote, watu wanaona jinsi ambavyo mifumo ya kiuchumi na kisiasa imewakatisha tamaa.

Simu za kisasa na za hali ya juu, Intaneti, na taarifa za habari ambazo hutolewa saa 24 zinafanya matukio yaliyotokea hata katika sehemu za mbali sana yawachochee watu katika maeneo mengine mengi.

Lakini maandamano yanatimiza nini? Watu wanaounga mkono maasi ya kijamii wanadai kwamba maandamano yametimiza mambo mengi ambayo hayangetimia bila maandamano.

Wao wanadai kuwa maandamano yameleta faraja kwa kwa maskini. Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, kufuatia ghasia zilizotokea katika mji wa Chicago, Illinois, Marekani kwa sababu ya kuongezeka kwa kodi ya nyumba wakati wa ule Mdororo Mkubwa wa Kiuchumi wa miaka ya 1930,vwasimamizi wa jiji waliacha kuwafukuza wapangaji na wakafanya mipango ili baadhi ya wafanya ghasia wapate kazi.

Maandamano kama hayo katika jiji la New York City yalifanya wapangaji 77,000 waliokuwa wamefukuzwa kutoka nyumba zaowarudishwe.

Wengine wanadai kuwa maandamano yametatua ukosefu wa haki. Hatimaye, ule mgomo wa mwaka wa 1955/1956 wa kukataa kupanda mabasi ya jiji huko Montgomery, Alabama, Marekani ulifanya sheria kuhusu ubaguzi wa rangi kwenyemabasi ziondolewe.

Wengine wanadai kuwa maandamano yamesimamisha miradi ya ujenzi. Desemba 2011, kwa sababu ya wasiwasi kuhusu uchafuzi wa mazingira, makumi ya maelfu ya watu waliandamana kupinga kujengwa kwa mtambo wa kutokeza umeme unaotumia makaa ya mawe karibu na Hong Kong, kwa hiyo ujenzi huo ulifutiliwa mbali.
Hata hivyo, si kila mara waandamanaji hupata wanachotaka. Kwa mfano, huenda viongozi wakawaadhibu badala ya kuwatimizia matakwa yao. Hivi karibuni rais wa nchi moja huko Mashariki ya Kati alisema hivi kuhusu harakati za maandamano huko: “Ni lazima tuwachukulie hatua kali,” na maelfu walikufa katika maasi hayo.

Hata waandamanaji wakitimiza malengo yao, matokeo ya maandamano huleta matatizo mapya. Mtu mmoja aliyesaidia kumtoa madarakani kiongoziwa nchi moja Afrika aliliambia hivi gazeti ‘Time’ la Marekani kuhusu utawala mpya: “Ulikuwa ushindi ambao mara moja uligeuka kuwa machafuko.”
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo