Fidelis Butahe, Dodoma
Freeman Mbowe |
MWENYEKITI wa Bunge, Musa Azan Zungu amemwomba radhi
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kwa kushindwa
kutambua mchango wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa Bunge,
alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya kubanwa na wabunge wa Chadema, Mwita
Waitara (Ukonga) na Pascal Haonga (Mbozi), ambao waliomba Mwongozo wakihoji
sababu za Mwenyekiti huyo kutaja watu waliotoa msaada wa waathirika hao na
kushindwa kumtaja Mbowe.
“Nikubali sikumtaja na nimwombe radhi kwa sababu
alihusika. Hili suala lisitugawe litufanye tuwe kitu kimoja,” alisema Zungu
baada ya kusikiliza hoja za wabunge hao.
Katika Mwongozo wa kwanza, Waitara alisema Zungu wakati
akitaja waliotoa msaada na kufika eneo la tukio kuwajulia hali waathirika wa
tetemeko hilo, alimtaja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitambua wazi kuwa
baada ya kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni kuondoka, Mbowe
alikwenda mkoani humo kutoa msaada.
“Sisi wabunge wa upinzani tumechangisha fedha na
kumkabidhi kiongozi wa upinzani azifikishe sehemu husika ili kusaidia waliopata
maafa haya. Naomba Mwongozo wako tunapopongezana na wewe humtaji kiongozi
mkubwa wa upinzani maana yake nini?” Alihoji Waitara.
“Si jambo jema, pia kumekuwa na malalamiko ya
kutotambuliwa kwa mameya na wabunge wa upinzani wanaohudhuria matukio ya
kitaifa.”
Haonga naye aliomba Mwongozo kama huo, kubainisha kuwa
kitendo hicho ni dharau kwa kiongozi huyo wa upinzani bungeni.
Awali Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) aliomba
Mwongozo juu ya wabunge kutuhumiwa kuhongwa fedha baada ya gazeti la kila
sikumnukuu Mbunge wa Manonga (CCM), Seif Gulamali, akisema wabunge wanahongwa
ili kutetea hoja bungeni.
Katika Mwongozo huo, Selasini alisema jambo hilo
likiachwa linaingilia Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kumtaka Mbunge huyo
kuwataja kwa majina wahusika ili kuondoa dhana ya wabunge wote kuhusishwa na
jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment