William Shao
|
Hii peke yake inamaanisha kuwa ukisema uongo lazima uupe ubongo
wako kazi kubwa ya kuweka kumbukumbu ya yale uliyoyasema, tofauti na mtu
anayesema kweli.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani wamegundua
kuwa ubongo unalazimika kufanya kazi kubwa na kwa bidii zaidi unaposema uongo kuliko
unaposema ukweli.
Profesa Mtafiti wa Magonjwa ya Akili na Mtafiti wa Masuala ya
Sayansi katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Dk Daniel Langleben, amekuwa
akilifanyia utafiti jambo hilo kwa miaka kadhaa kwa kutumia mashine ya fMRI (magnetic resonance imaging)
kubaini ni sehemu gani za ubongo zinazochochewa wakati mtu anaposema uongo.
Aligundua kuwa wakati tusemapo uongo, ubongo unahitaji kwanza
kuanza kazi ya uchakataji. Kisha, “Kwa kutumia silika, kwanza mtu mwongo
ataanza kufikiria jawabu la kweli kabla hajafikiria kuongea uongo,” linaandika
gazeti The News la Mexico City.
“Katika ubongo huwezi kupata kitu cha bure. Mchakato wa ubongo wa
kusema uongo ni mgumu zaidi kuliko mchakato wa ubongo wa kusema ukweli, na
unasababisha matumizi makubwa zaidi ya nyuroni (seli za neva),” anasema Dk
Langleben.
Ongezeko la ziada la matumizi ya nyuroni katika ubongo yalionekana
katika mashine ya fMRI kama glopu ya
umeme. “Hata kwa mtu ambaye hasemi uongo sana, uongo bado ni kazi ngumu kwa ubongo
wake,” likaandika gazeti hilo.
Hata hivyo, Taasisi ya Kisayansi ya Marekani, katika jarida Scientific American Mind la Septemba 2011,
iliandika: “Kwanza unalazimika kutunga hadithi (ya uongo), pili utalazimika
kuukumbukautunzi wako na tatu utalazimika kuhakikisha unaaminika kazi ambazo
zinahitaji matumizi makubwa ya ubongo.”
Aidha, mwandishi Mmarekani, Mark Twain (1835-1910), katika kitabu Adventures of Huckleberry Finn © 1884,
aliandika: “Ukisema kweli huna haja ya kukumbuka chochote.” Kwa maana hiyo, mwongo
anaupa ubongo wake mzigo mkubwa kuliko ilivyofikiriwa awali.
0 comments:
Post a Comment