JAJI Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande (pichani) amesema Sheria ya Mahakama ya Mafisadi imeanza kufanya kazi ikiwamo majaji 14 watakaofanya kazi, taratibu za kiutendaji na kesi za mafisadi zitachukua miezi tisa kusikilizwa na kutolewa hukumu.
Jaji Chande
alisema hayo jana Dar es Salaam ambapo alieleza pia kwamba katika mpango
mkakati
wa Idara ya
Mahakama wa kipindi cha miaka mitano jumla ya Sh bilioni 238 zinatarajiwa kutumika
kuboresha mahakama zote nchini, kwa lengo la kutoa haki kwa kila Mtanzania
atakayefika mahakamani.
“Kwa ufupi
tumeanza kazi, shauri lisizidi miezi tisa kusikilizwa, kama kutatatokea sababu
ambazo hazizuiliki, itaongezwa miezi sita ya kumaliza shauri hilo:
“Kama
zitatokea tena sababu ambazo haziepukiki, Mahakama imepewa iangalie muda
iliyopewa, lakini kinachotakiwa ni uwajibikaji na tutaangalia nani anakwamisha
ili tumchukulie hatua,” alisema Jaji Chande.
Alisema
kesi hizo hazitakuwa zikiahirishwa bila sababu ya msingi tofauti na
ilivyozoeleka sasa. “Tunataka kuangalia nani anakwamisha, hata kama Jaji
anakwamisha atachukuliwa hatua,” alisema Jaji Mkuu na kusisitiza:
“Naweza
kusema kuwa Mahakama hiyo imeanza kazi, kwa sababu sheria yake iko tayari na
kanuni zake zilitolewa Septemba tisa kupitia Tangazo kwenye Gazeti la Serikali GN
20,” alisema Jaji Chande.
Alifafanua,
kwamba kanuni hizo zinaelekeza jinsi mtu anavyofungua kesi, ambapo
zikishafunguliwa siku hiyo hiyo atapewa Jaji ambaye ndani ya siku 30 atafanyika
usikilizwaji wa awali kujua kama washitakiwa watakana makosa yao au watakiri.
Kuhusu
majaji ambao watasikiliza kesi hizo, alisema majaji 14 wamechaguliwa na
wamemaliza mafunzo na wapo katika masjala mbalimbali za Mahakama.
Mpango
mkakati
Akizungumzia
mpango huo, Jaji Chande alisema mpango huo ulishaanza kufanyika kwa Mahakama ya
Tanzania kufanya tathmini juu ya hali ya Mahakama na utoaji haki kwa watu
wanaopeleka kesi mahakamani.
Alibainisha
kuwa mpango huo ndio utakuwa dira yao ya kupanga mambo yao,ambapo wanatarajia
kutumia Sh bilioni 140 sawa na dola milioni 65 za Marekani lengo likiwa ni
kuboresha utoaji haki kwa watu na pia kuwafanya watu wawe na imani na Mahakama,
kwa sababu hivi sasa wengi hawana.
Alisema
mpango huo una nguzo tatu, ambayo ni matokeo makubwa manane na malengo 17, kwa
sababu ukiwa na mpango mkakati lazima ujue unafanya nini, ambapo nguzo ya
kwanza ni utawala bora na uwajibikaji.
Pia alisema
ipo na fursa ya kutoa na kupata haki na uharakishaji wa mashauri na kuongeza
imani ya wananchi juu ya mahakama, kama wajibu wake wa kutenda haki
unavyoeleza. Jaji Chande alisema Mahakama ilijipima kwa kuweka dira kwa sababu
hakuna taasisi ambayo itapata maendeleo bila dira, ambapo dira ni mtu yeyote
anayepeleka kesi apate haki sawa.
Alisema pia
wataongeza ubora wa hukumu, usuluhishi ili watu waelewane na mkataba uandikwe
uachwe mahakamani na kuimarisha ukaguzi wa mahakama zote kuanzia za mwanzo.
Jaji Mkuu
alisema mkakati huo pia utasaidia huduma za kimahakama ziende kwa teknolojia,
kwa sababu wanataka ifike hatua watu wafungue kesi kwenye mitandao na isaidie
majaji na mahakimu kutoandika kwa mikono.
Alisema
hadi sasa Mahakama ya Rufaa ambayo ndiyo kubwa, majaji wanatumia mikono
kuandika wakati nchi zingine kitu kama hicho hakipo.
Alibainisha
kuwa fedha hizo asilimia 60 zitatumika kuboresha miundombinu. Mradi wa
Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao ni mradi wa Benki ya Dunia ndiyo utashughulikia
maboresho hayo.
Alisema
uzinduzi wa mpango huo utafanyika Kibaha, Pwani, Septemba 21 na Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais John Magufuli, ambapo huko ndiko
wataeleza fedha zilizotolewa na Rais zilifanya nini.
Jaji Mkuu
alisema Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikiwasahau, lakini hivi sasa inawapa
kipaumbele ili kuhakikisha haki inapatikana.
0 comments:
Post a Comment