IGP Mangu |
JESHI la Polisi limeanza msako wa kukamata watu wanakwenda kulala nyumba za wageni muda wa kazi.
Msako huo ambao unaoelezwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda alilolitoa kwa wakuu wa wilaya jijini humo ulianza
juzi Tegeta, Kinondoni.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa JAMBO LEO ambaye
alishuhudia tukio la watu kukamatwa katika moja ya nyumba za wageni wakati hayo
yakitokea walidhani wanaokamatwa ni wahalifu au majambazi, lakini walivyohoji
walielezwa kuwa polisi walivamia nyumba hiyo ya wageni na kusomba watu wote waliokuwa
wamelala saa za kazi.
“Juzi nilikuwa Tegeta nikaona gari la Polisi linasomba
watu kutoka moja ya nyumba za wageni kwa kuwa walikuwa wengi tukadhani
majambazi lakini tulivyouliza, wakasema ni watu wanaolala mchana bila kufanya
kazi,’’ alisema mtoa habari huyo.
Alisema baadhi ya watu walijaribu kuhoji baada ya Polisi
kuondoka kutokana na kuhofia kuchanganywa katika kundi la watu wasiofanya kazi,
ndipo wakaelezwa kuwa ni agizo la Makonda kwamba wanaolala na kufanya ngono
muda wa kazi wakamatwe.
DC Kinondoni
JAMBO LEO lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali
Hapi ili kupata ufafanuzi kuhusu agizo hilo linalodaiwa kutolewa na wakuu wa
wilaya baada ya kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema:
“Watafutwe polisi.”
Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya hakukubali wala kukanusha
kuwepo kwa operesheni hiyo, lakini akasema suala lolote la kukamatwa watu
polisi ndio wanaopaswa kulitolea maelezo.
“Sasa huyo aliyekamatwa akiwa amelala hafanyi kazi na
aliyekusimulia pia walipaswa watoe majibu ya kina, alipaswa kwanza kuulizwa
yeye hilo suala na kama amekamatwa na polisi ufafanuzi unapaswa kufanywa na
Jeshi hilo si mimi,’’ alisema.
Kamanda wa Jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Simon Siro alikiri kuwepo kwa operesheni hiyo jana asubuhi katika kipindi cha
Joto la Asubuhi kinachorushwa na Redio ya Efm.
Siro alisema operesheni hiyo inalenga watu wanaozurura na
wasiojituma muda wa kazi.
0 comments:
Post a Comment