Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya |
Akiuliza swali bungeni jana, Mbunge huyo alisema,
Serikali ilifanya ukaguzi kwenye vyama vya ushirika mkoani humo pamoja na Chama
Kikuu cha Ushirika (WETCU) tangu mwaka juzi na kubaini ubadhirifu mkubwa wa
viongozi hao na benki mbalimbali.
“Kwa nini mpaka leo ripoti hiyo haijawekwa wazi, pia
vyama vingi viko kwenye hali mbaya na havikopesheki na hivyo kusababisha
wakulima kukosa pembejeo za kilimo, Serikali ina mpango gani mahususi wa kusaidia
vyama vya ushirika kwa kuzingatia mchango wa tumbaku kwenye uchumi wa Taifa
hili?” Alihoji Sakaya.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole
Nasha alisema ripoti ya ukaguzi ilishakabidhiwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini kupitia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora tangu Septemba 18, mwaka
juzi kwa Lengo la kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makosa ya jinai
yaliyobainika.
“Hadi Juni, maombi ya kuwafungulia mashitaka watuhumiwa
yalishapelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP) akiridhia
wafunguliwe mashitaka itafanyika hivyo,” alisema Nasha.
0 comments:
Post a Comment