Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman |
Katika mahakimu hao, wamo wa ngazi ya wafawidhi, mahakimu
wa mahakama za mwanzo za Rombo, Temeke, Bahi na Chamwino.
Jaji Chande alisema hayo, Dar es Salaam jana, baada ya
kukabidhiwa ripoti ya utendaji kazi wa Mahakama na wasajili kuanzia Januari
hadi Agosti, kutokana na kujiwekea utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kwa
uwazi.
Alisema watumishi hao walifukuzwa kazi Agosti 18, baada
ya kikao cha Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo ndiyo ya nidhamu kukaa na
kutoka na uamuzi.
“Tumefukuza kazi watumishi 34 kutokana na makosa ya utovu
wa nidhamu ambapo mahakimu ni 11 na maofisa wengine 23 wa Mahakama.
“Lakini pia mfahamu hii ni idadi ndogo ya watendaji ya
Mahakama, ambapo Machi tulikuwa na watendaji 6,406 na waliofukuzwa kazi 34 ni
asilimia 0.005, ambao ni wafanyakazi wachache, lakini kwa Mahakama ni doa kuwa
na mahakimu au watendaji wenye kasoro au dosari,” alisema Jaji Chande.
Alisema walifikia hatua hiyo kwa mmoja wa mahakimu hao
aliyetumia muhuri wa Mahakama kinyume na utaratibu na sheria kwa masuala binafsi,
hili ni kosa la kinidhamu, kwa hiyo alifunguliwa mashitaka mashahidi wakaitwa
na Kamati ya Maadili ikaamua na Tume ikathibitisha wakafukuzwa kazi.
Alisema mwingine alichangia kusaidia mtu kufungua kesi
moja kwenye mahakama mbili tofauti, ambayo hiyo iliathiri utendaji haki kwa
kutolewa hukumu mbili katika kesi moja.
Pia alisema hakimu mwingine alifungua shauri la mirathi
bila hati ya kuthibitisha kifo, mashitaka yake yalithibishwa kwa kiwango kinachotakiwa
na kuchukuliwa hatua ya kufukuzwa kwa sababu ni makosa ya kinidhamu.
Alifafanua kuwa kuna makosa ya kisheria ambayo hakimu au
jaji hawezi kuchukuliwa hatua kama alijichanganya katika vifungu vya sheria,
lakini katika mzaha wa sheria hao ndio wanapelekwa katika kamati za maadili kwa
kukosa sifa.
Mahakimu viporo
Alibainisha kuwa wapo mahakimu 28 au 30 walioshinda kesi
za rushwa, lakini Tume ikaona kwamba kutokana na tuhuma kuwa nzito ipo haja ya
kuwajadili ili waone hatima yao.
Alisema wamefanya hivyo, kwa sababu tayari kuna vitendo
vya utovu wa nidhamu kwa hiyo ni lazima wakae na kuamua ni hat-ua gani
wachukuliwe kwa sababu walishaingia doa.
Jaji Chande alisema mahakimu wengine 32 walishinda kesi
za jinai, lakini ni vema wawafungulie mashitaka ya maadili, bila kujali
walishinda mashitaka ya jinai.
0 comments:
Post a Comment