Spika wa Bunge, Job Ndungai |
Ingawa hakutaja chama alichokilenga, hivi karibuni Baraza
Kuu la Uongozi la CUF lililokutana Zanzibar, lilimsimamisha uanachama Mbunge
wake wa Kaliua, Magdalena Sakaya kutokana na kilichoelezwa ni kuvunja Katiba
kwa kutohudhuria kikao bila taarifa.
Mbunge mwingine aliyekumbwa na rungu hilo ni Maftaha Nashuma
(Mtwara Mjini), aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na
wanachama wengine wanane.
Akizungumza baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu
bungeni jana, Ndugai alisema: “Vyama vya Upinzani vimekuwa na utaratibu wa kufukuza
wabunge wao, ningependa vyama hivi vijifunze kutoka CCM ambacho sijawahi
kusikia kikifukuza mbunge miaka ya karibuni.”
Ndugai alisema kitendo cha CCM kutofukuza wabunge wake
hakimaanishi kuwa wawakilishi hao wa wananchi ni malaika, kwamba wapo vichwa
ngumu.
“Hawafukuzi hovyo maana kupata mbunge wa kuchaguliwa ni
shughuli pevu. Mbunge si lazima achaguliwe na wanachama wa chama husika, pia
anaweza kuchaguliwa na wananchi wengi lakini ninyi mnakaa wachache na
kumfukuza,” alisema.
Alisema kitendo cha mbunge kufukuzwa kinasababisha
gharama kubwa kumpata mwingine, huku akiomba radhi kwa kauli yake hiyo baada ya
wabunge wa Upinzani kuonekana kukerwayo.
“Nimeomba radhi mapema msinishambulie nitoe tu mawazo
yangu, ni vizuri tukipata mbunge tuvumiliane naye, haya mambo madogo madogo si
tumalize huko ndani (ya chama) na katika hili muiige CCM maana inafanya
mazuri,” alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment