Leonce Zimbandu
WAZIRI
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amepokea msaada wa Sh.
bilioni 6.3 kutoka Shirika la Misaada la Uingereza (DFID) kwa ajili ya ujenzi
wa Sekondari ya Ihungo, Bukoba mkoani Kagera.
Ujenzi
wa shule hiyo unatarajiwa kuanza mara moja chini ya Wakala wa Majengo ya
Serikali (TBA) ili kutekeleza masharti ya msaada wa kujenga shule ya kisasa
itakayohimili tetemeko la ardhi.
Profesa
Ndalichako (pichani) alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Alisema
DFID pia imeonesha nia ya kujenga nyumba 10 za walimu wa sekondari ya Rugambwa,
hali hiyo ikionesha Uingereza kuguswa na tukiohilo.
“Nimeona
niwaite leo ili kuzungumzia msaada ambao Serikali imepokea kutoka DFID kwa
ajili ya kujenga shule ya Ihungo ambayo inatarajiwa kukamilika Januari,” alisema.
Alisema
shirika hilo lilifikia hatua hiyo baada ya ujumbe wake kutembelea waathirika wa
tetemeko la ardhi lililotokea Kagera Septemba 10.
Profesa
Ndalichako alifafanua kuwa michoro ya ramani ya shule hiyo imekamilika ambayo
inahusisha ujenzi wa maabara na vyumba vya kisasa vya madarasa.
Mkuu wa
DFID Tanzania, Vel Gnanendran alisema baada ya kutembelea Kagera walijionea
namna watu walivyoathirika na tetemeko hilo. “Uingereza kupitia DFID imeamua
kutoa msaada wa kuijenga shule hiyo na nyumba 10 za walimu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment