SIKU nne tangu madereva 15 wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na waasi wa kundi MaiMai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamesimulia walivyoishi na waasi hao kambini na jinsi walivyofanikiwa kuwatoroka.
Wakizungumza
jana katika mahojiano maalumu na JAMBO LEO wakiwa nchini Congo, walisema walikuwa
wakilazimika kusota wakitumia tumbo kwa mwendo mrefu msituni, baada ya kuamriwa
na askari hao ili kukwepa wasionekane na majeshi ya Serikali ya nchi hiyo
wanayopambana nayo.
Mmoja wa
madereva hao, Amdani Zarafi (41) ambaye alishikiliwa na waasi hadi kwenye kambi
yao, alisema walitumia wastani wa saa kumi njiani kabla ya kufika kwenye kambi
hiyo ambako kila dereva aliamriwa kupiga simu kwa bosi wake na kumweleza kilichotokea.
“Tulianza
safari kuelekea porini saa 2:00 asubuhi baada ya kuchomewa magari na tulifika
kwenye kambi yao saa kumi jioni. Mwendo ulikuwa ni mchaka mchaka tu, ulikuwa ni
pori kwa pori,” alisema Zarafi.
Alisema
walipofika kambini waliendelea kuwekwa chini ya ulinzi huku simu, leseni, fedha
na funguo za magari wakiwa wamenyang’anywa na waasi hao.
Aliongeza
kuwa waasi hao waliwaamuru kuwa watulivu huku wakisisitiza ombi lao kwa kila
mmoja kuzungumza na bosi wake na kumweleza hali halisi kwamba wanatakiwa kulipa
Dola 4,000 za Marekani kila mmoja ili aachiwe.
Alisema
waasi hao walitoa angalizo kwa mabosi wao kwamba endapo taarifa zitafika kwa
wanajeshi wa Jeshi la DRC na wao kufuatwa walipojificha, basi madereva hao
wangeuawa.
Zafari
alisema wakati wakiwa porini siku ya pili huku wakiendelea kuwasiliana na
mabosi wao wale waasi walimtuma mmoja wao kwenda mjini kununua unga kwaajili ya
kuwalisha madereva
hao.
“Wakati
yule muasi akirudi kutoka kununua unga, wanajeshi wa DRC ambao walikuwa
wanatufuatilia walimuona na kuanza kumfuatilia nyuma hadi wakafanikiwa kufika
kambini,”alisema na kuongeza:
“Wakati
akiwa njiani kuja kambini, yule muasi aliwaona wale wanajeshi akawa anakimbia
na alipofika tu kambini aliwaambia waasi wenzake kambi imevamiwa na wanajeshi.
Walipoambiwa hivyo, wale waasi walituamuru tuondoke hapo na kuwafuata watakako kwenda,
ikabidi tuaze kuwafuata baada ya muda tukasikia risasi zinalia tukaanza
kukimbia nao.
Alisema
baada ya hapo tulitawanyika kila mmoja kwake wale wanajeshi wakaendelea kupiga risasi
na waasi wakakimbia ndipo wanajeshi wakawaokoa madereva na kuwahifadhi kwenye kambi
yao ya jeshi.
Naye
Kumbuka Suleimani (40) ambaye alifanikiwa kutoroka mikononi mwa waasi hao,
alisema walitembezwa umbali mrefu kukatisha misitu hata kulala njiani ili
kufika kwenye pori lingine ambalo ni maficho ya waasi hao.
0 comments:
Post a Comment