Peter Akaro
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka amezungumzia Tuzo
ya Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), na kuweka bayana
kwamba sakata la Escrow ndiyo sababu ya kutopokea dola 100,000 za Marekani za
Tuzo hiyo.
Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 New York, Marekani ambayo mfadhili
wa Tuzo ni Waziri Mkuu wa Bahrain, Mwana Mfalme Khalifa bin Al Khalifa.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa
UN imeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambayo imekuja kupisha malengo
17 ya milenia ambayo wakati yanaanzishwa alikuwapo, hivyo watoa tuzo walitambua
ushiriki wake.
“Tuzo hizi si za kuomba, watu hukaa na kupendekeza mtu wa kupewa na
hii ni mara ya pili, mara ya kwanza nilipewa mwaka 2009 Sweden,” alisema na kuongeza:
“Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii unayotoka au kuitumikia na
kufanya nayo kazi, hivyo wametambua mchango wangu katika kutumikia wananchi wa Muleba,”
alisema.
Aidha, Profesa Tibaijuka alitaja sababu zilizopokea yeye kutochukua
dola 100,000 za Tuzo hiyo. “Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta mapema,
kulikuwa na uwezekano wa kuichukua, lakini nikasema kwa hali halisi ya
nyumbani, hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi
nikaiacha mezani wao wafanye wanavyotaka,” alisema.
0 comments:
Post a Comment