MWANAMUME anayehisi kwenda haja ndogo mara kwa mara au kushindwa
kuimaliza, anapaswa kuchunguzwa ili kujua kama anaugonjwa wa tezidume.
Daktari wa Magonjwa ya Binadamu, Dk Stephen Kisaka amesema mwenye
tezidume asipotibiwa mapema, anaweza kupata matatizo ya kiafya kama ya figo,
kibofu cha mkojo na shinikizo la damu.
Matatizo mengine, alisema ni kushindwa kutoa mbegu za kiume wakati
wa tendo la ndoa, damu kuganda, maambukizi ndani ya njia ya mkojo na homa ya
mapafu. Dk Kisaka alisema ugonjwa huo ukibainika mapema ni rahisi kuutibu au
kuudhibiti.
Hata hivyo, alisema watu wengi huchelewa kwenda hospitali na matokeo
yake hujikuta wakiathirika
kiafya, kwa sababu wakati huo tiba inachukua muda mrefu au
kulazimika kufanyiwa upasuaji. Katika maelezo yake, Dk Kisaka alieleza namna ya
kujikinga na mambo ambayo mwanamume anapaswa kuepuka ili asipate tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment