Suleiman Abeid, Shinyanga
Mkutano wa Chama cha Mapinduzi |
WANACHAMA 16 wa
jumuiya za CCM mkoani hapa wamejitokeza kuwania uenyekiti wa mkoa ndani ya
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) na Jumuiya
ya Wazazi (WAZAZI).
Kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari jana mjini hapa na makatibu wa
jumuiya hizo, uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa ngazi ya wilaya, mkoa na
Taifa, ulifungwa rasmi Julai 10 saa 10 jioni.
Katibu wa UVCCM wa
Mkoa, Teddy Salum alisema vijana wanane wamejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti
mkoa wa jumuiya hiyo na wengine wanane wakiwania ujumbe wa Baraza Kuu Taifa.
Teddy alitaja
waliojitokeza kugombea uenyekiti mkoa kuwa ni, Lucas Magadula, Baraka
Shemahonge, Jimotoli Maduka, Maduhu Shiwa, Joseph Jilala, Abel Kaholwe, Hassan
Ramadhan na Stambuli Mwombeki huku Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Reuben
Shigela akishindwa kutetea kiti chake kutokana na umri.
Aliwataja
waliojitokeza kugombea ujumbe wa Baraza Kuu Taifa kuwa ni Elikana Machanya,
Abdul Ngoromole, Joseph Segagi, Robert Masuka, Abdulrahman Nyerere, Janeth
Seni, Clement Madinda na Adili Kombolela.
Kwa UWT
waliojitokeza kuwania uenyekiti wa mkoa, ni pamoja na Mwenyekiti anayetetea
kiti chake, Angela Paulo na Zipora Pangani aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya.
Katibu wa UWT wa
Mkoa, Angela alitaja wagombea wengine kuwa ni Margareth Abwolo, Jackline
Bulay na Christina Kija na waliojitokeza kuwania ujumbe wa Baraza Kuu Taifa la
UWT, ni pamoja na Dk Christina Mzava, Joyce Masunga, Mariamu Nyangaka na Ruth
Kibela.
Katibu wa WAZAZI
Mkoa, Masanja Salu alisema mpaka siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu ni
wagombea watatu tu ndio waliorejesha wakiomba kugombea uenyekiti wa mkoa wa
Jumuiya hiyo.
Salu aliwataja
waliorejesha fomu kuwa ni Perer Sheria, Alhaji Salum Abdalah na Ibrahimu Kani huku
Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Willy Mzava akitangaza mapema kujitoa.
0 comments:
Post a Comment