Mwandishi Wetu
Kamanda Mpinga |
MAAGIZO ya Rais John Magufuli kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon
Sirro yameanza kutekelezwa. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana Mkuu huyo
wa Polisi kufanya mabadiliko yaliyogusa wadhifa wa kitaifa kwenye Jeshi hilo.
Katika mabadiliko hayo, IGP Sirro amemng’oa kwenye nafasi yake aliyekuwa
Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na kumteua kuwa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza baada ya kumwapisha Sirro hivi karibuni Ikulu, Dar es
Salaam, Rais Magufuli alimtaka kusafisha Jeshi hilo lililokumbwa na changamoto za
kiutendaji yakiwamo matukio ya ujambazi na mauaji ya askari wake na raia
Kibiti, Pwani.
Taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa jana na Msemaji wake, Barnabas
Mwakalukwa ilisema Sirro amembadilisha kituo cha kazi na nafasi yake inachukuliwa na
Fortunatus Musilimu ambaye alikuwa Mkuu wa Operesheni kwenye kikosi hicho.
Kabla ya uteuzi huo wa jana, Musilimu alikuwa akikaimu nafasi aliyokuwa nayo
Mpinga huku ikielezwa kuwa Mkuu huyo wa zamani wa Trafiki alikuwa likizo.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya, Dhahiri Kidavashari, amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
Hata hivyo, Msemaji huyo wa Polisi alisema uhamisho huo ni wa kawaida
katika alichoeleza kuwa ni kuboresha utendaji kazi zao kwa mujibu wa kanuni,
taratibu na miongozo ya Polisi.
Mpinga alipotafutwa kuzungumzia mabadiliko hayo, simu yake iliita muda
mrefu bila majibu.
hicho kwa zaidi ya miaka mitano na nyota yake iling’ara alipokaimu akiwa
na aliyekuwa Mkuu wa Kikosi hicho, marehemu James Kombe.
Alipotakiwa kuzungumzia uamuzi wa Sirro kumpandisha cheo aliyekuwa Musilimu,
alisema atazungumza baada ya kukabidhiwa ofisi na kwa sasa aachwe kwanza.
“Ndiyo nimejua leo, jamani niacheni nikabidhiwe ofisi ndipo nitazungumza
mikakati yangu. Bado mwenzangu yuko ofisini,” alisema.
0 comments:
Post a Comment