Mwandishi Wetu, Lindi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa |
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji
cha Mnolela mkoani hapa kwa muda mfupi.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo
ya kisasa ulianza Machi na sasa umekamilika, jambo ambalo litarahisisha
upatikanaji huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na jirani.
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo juzi alipozungumza na
wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na
NHC.
Alisema
ujenzi wa zahanati hiyo ni mwendelezo wa mkakati wa Serikali kuboresha huduma
za afya kwa kuzisogeza karibu na wananchi.
“Rais
John Magufuli amedhamiria kuondolea wananchi changamoto za huduma za afya,
hivyo tuendelee kumwunga mkono,” alisema Waziri Mkuu.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo
ulisimamiwa na shirika lake kwa Sh milioni 65.5.
“Sh
milioni 15 zilitolewa na Rais, Sh milioni 10 na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye
huku NHC ikitoa Sh milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa Halmashauri,”
alisema.
Awali
Nape alimshukuru Rais Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa kwenye ujenzi wa
zahanati hiyo.
Nape
alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakazi wa kijiji cha Mnolela na wananchi
wengine wanaoishi maeneo jirani.
0 comments:
Post a Comment