MTENDAJI Mkuu wa Kampuni ya Quality Group,
Arif Sheikh ametunukiwa Tuzo ya Kiongozi Mkuu-Fahari ya Taifa la India Mwaka
2016.
Sheikh ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la
Utawala la Kampuni hiyo kubwa nchini Tanzania, ametukiwa tuzo hiyo juzi
(Septemba 3) mjini Mumbai, India.
Amepata tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya
The Asia One Global Indian Leader, baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu
katika kubadili taswira ya sekta ya biashara nchini Tanzania.
Mbali na Sheikh, wengine waliopata tuzo hiyo
ni Mwanzishili wa kampuni ya Dangote - Aliko Dangote, Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Pepsi, Indira Nooyi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Microsoft, Satya Nadela.
Pia, taasisi hiyo ikawatambua na kuwapa tuzo
hiyo, Nita Ambani, Mshindi wa tuzo ya Nobeli, Prof Amartya Sen, Gautam
Singhania na Raymond Group.
Kwa
nini Sheikh?
Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh
aliwashukuru wafanyakazi wenzake wa kampuni ya Quality Group Limited, hususan
mtangulizi wake katika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Yusuf Manji.
“Imekuwa ni heshima kubwa sana kwangu kupata
tuzo hii ya kimataifa. Ingawa mimi ndiye niliyepewa tuzo hiyo, ninaitoa kuwa
ni fahari ya kampuni ninayoiongoza ya Quality Group Limited. Nimefurahi kwamba
nimeingia katika orodha ya watu waliowahi kupata tuzo hiyo ambao nimekuwa
nikivutiwa nao sana.”
Sheikh alisema ametembea na kufanya kazi
katika mabara mbalimbali, lakini kote hajaona kiongozi anayemvutia kama Rais
John Magufuli ambaye ameapa kumuunga mkono katika jitihada zake mbalimbali za
kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.
Mashuhuda
wasema
Mmoja wa watu waliohudhuria hafla hiyo
alitaja kilichomfanya Sheikh afanikiwe kupata tuzo hiyo kuwa ni uwezo wake wa
kuelimisha wengine kutumia taaluma zao kwa ajili ya kujiletea maendeleo
endelevu.
“Amekuwa akifanya shughuli zake kwa
kuwashirikisha wafanyakazi wenzake na ukiwauliza wafanyakazi wake watakwambia
kuwa kufanya kazi na Sheikh ni ngumu lakini inakusaidia kujifunza,” alisema.
Kwa sasa Sheikh anakuza kipawa chake cha
kuendesha biashara nchini Tanzania kwa kutekeleza miradi kadhaa ukiwamo mradi
wa FastaFasta unaotoa huduma ya usafiri kwa kutumia pikipiki 60,000 na mradi wa
kuendeleza Mji Mkongwe ambao utakapoingia katika hatua ya tatu, utakuwa moja
ya miradi michache inayotoa ajira kwa Watanzania wengi.
Miradi mingine ni Pamoja worlds ambao ni
mradi wa kwanza nchini Tanzania unaotoa huduma ya mtandao kwa Lugha ya
Kiswahili, biashara mtandao na miradi mingine kadhaa katika sekta zinazoendelea
kukua nchini humo ikiwamo sekta ya Elimu, afya, Teknolojia, mauzo ya nje,
Magazeti, Kilimo Biashara na uchimbaji wa madini ambazo kwa pamoja zimeleta
faida ya Dola Bilioni moja za Marekani
“Kwa pamoja miradi hiyo imeifanya Tanzania
kuwa ni nchi yenye fursa nzuri ya kukua kiuchumi, kukuza ajira pamoja na kuwa
eneo salama la uwekezaji wa kimataifa.”
0 comments:
Post a Comment