Mary Mtuka
Samia Suluhu |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan na
Mwenyeki wa Chama cha ACT – Wazalendo, Anna Mgwira wametajwa kuwa mashujaa
katika historia ya Afrika na Tanzania kwa mwaka 2015.
Ripoti ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa
Tanzania wa mwaka 2015 imewataja kinamama hao kuwa ni mashujaa kutokana na
ujasiri waliouonyesha katika kujitokeza, kushiriki na kusimamia nafasi walizogombea.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa na
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Asasi za Kiraia wa
kuangalia chaguzi Tanzania Mghwira na Samia walionesha uwezo mkubwa katika kampeni
za uchaguzi huo uliomwingiza madarakani mgombea wa CCM, John Magufuli.
Katika uchaguzi huo, Mghwira alikuwa
anawania Urais kupita chama hicho cha ACT-Wazalendo wakati Samia alikuwa
anasaidiana na Magufuli kutetea tiketi ya CCM.
Kampeni za kinamama hao zilionekana
kukonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wengi wa vyama vyao, hasa wanawake ambao
kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, walilaumiwa kumtelekeza mwanamke mwanzao
aliyewania Urais, Anna Senkoro.
Kilichofanu uchaguzi wa mwaka jana
unekane wa kipekee ni uamuzi wa CCM kumteua Samia mgombea mwenza akiwa mwanamke
wa kwanza kuwania nafasi hiyo tangu chama hicho kianze kusimamisha wagombea
wenza.
Hata hivyo, Mghwira na Samia siyo
wanawake wa kwanza Afrika na Tanzania kusimama kwenye kampeni za uchaguzi.
Baadhi ya wanawake waliowahi kusimama kwenye kampeni na nchi/vyama vyao kwenye
mabano ni Ellen Johnson (Liberia), Joyce Banda (Malawi) na Catherine Samba (Jamhuri
ya Kati).
Nchi zingine zilizowahi kuwasimamisha
wanawake katika nafasi za umakamu wa rais ni Uganda, Gambia, Zimbabwe, Afrika
Kusini na Burundi.
Anna Senkoro ndiye aliyekuwa mwanamke wa
kwanza Tanzania kuwania nafasi ya urais aliposimama mwaka 2005 kwa tiketi ya
PPT- Maendeleo kupambana na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM,
Jakaya Kikwete.
Alipata kura 18, 741 sawa na asilimia
0.1 ya kura zote zilizopigwa. Lakini mwenyewe na wanaharakati kadhaa wamekuwa
wakiwalaumu wanawake kuwa walimtelekeza mwenzao huyo kwa kutompigia kura.
0 comments:
Post a Comment