Bahati Othumani, Hai
Rais John Magufuli |
KANISA la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro limempongeza Rais John Magufuli kwa hatua mbalimbali za kiutendaji alizochukua kulinda maslahi ya taifa.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Askofu William Mollel, baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kanisa hilo katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wa Serikali.
Mollel alisema utendaji kazi wa Rais Magufuli unapaswa kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote kwani ameonyesha dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania kwa kutanguliza maslahi ya taifa kwanza pasipo kuangalia itikadi za kisiasa.
“Rais ameonyesha wazi dhamira yake ya kuleta maendeleo na kile
anachotaka kifanyike, anakisimamia kwa vitendo. Katika hili
tunampongeza sana na tutaendelea kumwombea awe na afya njema na hekima katika utendaji wake,” aliongeza Mollel.
Adha,
aliwahimiza wanasiasa kujenga utamaduni wa kutanguliza mbele uzalendo wa taifa
ili kuleta maendeleo.
Alisema suala la
maendeleo kwa Watanzania ni la kila mmoja bila kujali itikadi za sisa
kinachotakiwa ni kuweka maslahi ya taifa mbele kwa manufaa ya Watanzania
wote.
Katibu Mkuu wa
Kanisa hilo Tanzania, Askofu Unity Urasa alisema Rais Magufuli amefanya mambo
makubwa kwa muda mfupi madarakani akitaja suala la wamachinga kupata maeneo
mazuri pia wachimbaji wadogo kuwa mfano wa aliyopigania.
Kwa upande wakem,
Askofu wa Makanisa PEFA Kilimanjaro, Elieta Mbise alisema kanisa hilo linakemea
kwa nguvu zote mambo ya ukatili wa kijinsia ikiwamo ushoga,nakuwaomba
watanzania kuwa wachamungu ili kuachana na mambo hayo kwani yamekuwa
yakiongezeka siku hadi siku.
0 comments:
Post a Comment