Bahati Othumani, Moshi
Ponda Issa Ponda |
KATIBU wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Ponda Issa Ponda, ameishauri Serikali
kuwa na utaratibu wa kumaliza kesi mapema ili kuondoa mrundikano wa mahabusu
magerezani.
Ponda alisema
hayo Arusha baada ya kutembelea Gereza la Kisongo akifuatana na
wanasheria mbalimbali akiwamo Mwanasheria wa Jukwaa la Vijana wa Kiislamu wa Mkoa
wa Kilimanjaro, Idrisa Munisi kwa lengo la kuwajulia hali Waislamu kwenye
Gereza hilo kwa tuhuma za ugaidi.
Alisema Serikali
isipoharakisha kusikiliza kesi itaendelea kupata hasara kubwa ya kuwatunza na
kuathiri washitakiwa kwa kuwanyima haki yao ya msingi kwa wakati.
"Nimejionea
mwenyewe jinsi ya mrundikano wa kesi ambazo hazipatiwi ufumbuzi kwa wakati, jambo
ambalo si sahihi, ni vema Serikali ikaangalia namna bora ya kuharakisha
kumaliza mashauri yaliyo mahakamani," alisema Ponda.
Alisema ndani ya
gereza hilo, kuna wananchi wengi wanashikiliwa kwa mda mrefu bila kesi
kusikilizwa mahakamani na hawana watu wa kuwasemea, jambo hilo ni la hatari na
linajenga woga kwa wananchi.
Akiwa
Kilimanjaro kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Vijana wa Kiislamu uliofanyika
katika sekondari ya Mudio wilayani Hai, Ponda alitaka vijana hao kuwa wamoja na
kuacha kutenganishwa na madhehebu
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Vijana wa Mkoa wa Kilimanjaro, Abdalah Muhamedi alisema lengo la
kongamano hilo la siku tatu, lilikuwa ni kujadili mambo mbalimbali kuhusu dini
na pia ajira kwa vijana, jumla ya vijana 178 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania walihudhuria kongamano hilo.
Katibu Mkuu wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Shekhe Suleiman Lolila katika
sherehe za Maulid akizungumzia suala la ugaidi, alitaka Mahakama iharakishe
kusikiliza kesi za tuhuma za makosa ya hayo.
Alisema kufanya
hivyo kutasaidia raia wema wasio na kosa kuachwa huru na kuendelea na shughuli
zao.
0 comments:
Post a Comment