Suleiman Msuya
Profesa Mark Mwandosya |
“SINA cha kusema”. Hiyo ni kauli ya mwanasiasa
mkongwe, Profesa Mark Mwandosya, alipotakiwa kuzungumzia masuala ya kitaifa jana
akisema ukimya wake unatokana na kutokuwa na la kusema.
Mwandosya alitoa kauli hiyo baada ya
ukimya wa takriban mwaka mmoja tangu kumalizika kwa mchakato wa kutafuta
mgombea urais ndani ya CCM, ambapo wagombea zaidi ya 35 akiwamo yeye
walijitokeza na kuchujwa hatua za awali.
Mchujo huo uliibua malalamiko kutoka
baadhi ya wajumbe na baadhi kuamua kujitoa CCM akiwamo Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa aliyehamia Chadema.
Katika mchakato huo, Rais John Magufuli alipitishwa
na kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana akimshinda mpizani wake wa
karibu, Lowassa.
Lowassa aliwania nafasi hiyo kupitia
Chadema na kuungwa mkono na vyama vinne vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Tangu wakati huo, Mwandosya hajasikika
wala kuonekana kwenye majukwaa ya kisiasa.
Mara kadhaa gazeti hili lilimtafuta
kupata maoni yake kuhusu masuala mbalimbali lakini mara zote simu yake iliita
bila kupokewa.
Ukimya wa Profesa Mwandosya ulizua
maswali mengi, lakini jana alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia
pamoja na mambo mengine mwaka mmoja wa Serikali ya Rais John Magufuli na CCM,
alisema hana cha kusema.
“Mimi nipo kijijini kama unataka kujua
masuala ya kijijini kwangu niulize, hayo ya mwaka mmoja wa Magufuli na CCM sina
la kusema,” alisema.
Mwandosya anatajwa kama moja ya viongozi
waliofanya kazi kwa mafanikio huku akionesha utulivu na kujiamini kwa kila
jambo hasa bungeni, ambapo alikuwa akitumia usemi wa kisomi kuwataka wabunge
watoe hoja na si kufoka kwa jambo wasilolijua.
0 comments:
Post a Comment