Mkurugenzi SSRA aifunda mifuko ya Jamii


Warioba Igombe, Morogoro
Sarah Msika


MIFUKO ya Hifadhi ya Jamii nchini imetakiwa kuzingatia sheria ili kuondoa usumbufu kwa wanachama wao wakati wa kudai mafao ya kustaafu au kuachishwa kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Msika, alitoa rai hiyo wakati akizungumza na maofisa wote wa mifuko hiyo nchini juma lililopita.

Msika aliwataka maofisa hao kutimiza majukumu ya mamlaka kisheria ya kutoa elimu kwa umma pamoja na kutekeleza mpango na mkakati wa elimu wa mwaka 2014 ya hifadhi ya jamii ili kutatua changamoto katika mifuko hiyo.

“Napenda kutumia fursa hii kuwataka maafisa wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini kutekeleza mpango wa mamlaka ya mwaka 2014, kwani kufanya hivyo kutasadia kuondoa changamoto kwa wanachama dhidi ya mwajiri,” alisema Msika.

Alisema kama elimu ya hifadhi ya jamii ikitolewa kikamilifu mbali na kuwaelimisha wanachama, itawasaida maofisa hao kufahamu vyema wajibu na majumu yao ya kila siku.

Msika alisema lengo la SSRA ni kusimamia sekta ya jamii nchini na moja ya majukumu yake ni kuhakikisha inalinda na kutetea maslahi ya wananacha hivyo ni wajibu wa watendaji wa sekta hii kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na na ongezeko la malalamiko kutoka kwa wanachama hasa kuhusu masuala ya ujumlishaji vipindi vya uchangiaji ambapo wanachama wamejikuta wakichangia mfuko zaidi mmoja na kuleta usumbufu aliosema utaondolewa kwa kupewa elimu na mifuko ya hifadhi.

Mkurugenzi wa Huduma Kisheria wa Mamlaka ya Usimamizi wa Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole aliwataka waajiri kufuata sheria ya Mamlaka sura 135 kwani atakaeivunja atachukuliwa hatua za kisheria.

Njole alisema kuwa Sheria ya SSRA sura 135 inahitahi waajiri kutambua wajibu wao ili kuepusha ushubufu wa kudai mafao kutoka kwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo