Mwandishi Wetu
Dk Hassan Abbas |
SERIKALI imemwagiza Mhariri wa Gazeti la
MwanaHALISI, Jabir Idrisa kuchapicha barua ya kuomba radhi kwenye urasa wa
mbele wa gazeti hilo Februari 6 kama ilivyokuwa habari inayomhusisha Rais John
Magufuli katika toleo lililopita.
Agizo hilo lililotolewa jana na Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan
Abbas, baada ya kupokea barua ya kuomba radhi kutoka kwa Mhariri huyo kulingana
na maagizo aliyopewa na Maelezo.
Dk Abbas alisema alipokea barua ya
kuomba radhi iliyoandikwa na Mhariri wa MwanaHALISI akikiri upungufu katika
habari aliyochapisha akimhususha Rais Magufuli isivyo halali.
Habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha
habari: ‘Ufisadi ofisini kwa JPM’ kwa mujibu wa MAELEZO haikuwa na ukweli,
hivyo kuagiza kuombwa radhi.
Dk Abbas alisema pamoja na chombo hicho
kurudia makosa mara kwa mara, Serikali imezingatia ukweli kwamba safari hii
wahariri wa gazeti husika hawakufanya tashtiti. ”Wamekuwa waungwana, kwanza kwa
kukubali mwito, tofauti na ukaidi wa awali, na pili kukiri kosa,” alisema.
Aidha, Mkurugenzi huyo alisema Serikali
inatoa onyo kali na hatua kali zaidi zitachukuliwa iwapo wataendeleza uandishi
unaokiuka maadili ya kitaaluma na sheria za nchi.
Alisema Serikali itaendelea kuwa mlezi
wa taaluma hiyo muhimu na adhimu ya habari, lakini kamwe haitasita kuchukua
hatua dhidi ya wanaoacha kuandika ukweli na kuingiza hisia zao binafsi kwenye
taaluma.
Hivi karibuni Rais Magufuli alishutumu
baadhi ya vyombo vya habari kwa kupotosha habari, lakini bila kuvitaja akasema
kuna magazeti mawili yamekalia kuti kavu.
0 comments:
Post a Comment