Stephen Kidoyayi, Shinyanga
BAADHI ya watumishi na walinzi wa
Halmashauri ya Kishapu mkoani hapa, wanahojiwa na Polisi baada ya kuibwa vifaa
vinavyotumika kuhakiki vyeti kwa watumishi wa umma na kuandikisha vitambulisho
vya Taifa katika Kamanda
wa Polisi wa Mkoa, Muliro Jumanne jana
alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kueleza kwamba uchunguzi wa tukio hilo la wizi unaendelea.
Kwa mujibu wa Kamanda, vifaa viliyoibwa ni pamoja na kamera mbili
na viegesho vyake na vifaa hivyo vilipotea jana asubuhi wakati wakijiandaa
kuendelea na uhakiki wa vyeti na kuandikisha vitambulisho vya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba alisema vifaa
vilivyoibwa ni mali ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. (NIDA).
“Leo asubuhi Ofisa wa NIDA, alibaini kamera mbili na viegesha vyake
havionekani, tunaendelea kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
ili kubaini wahusika na kupata vifaa hivyo,” alisema Talaba.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen
Magoiga alisema vifaa hivyo vilikuwa vimehifadhiwa kwenye ofisi ya Halmashauri
kwa ajili ya kupigia picha za NIDA.
Baadhi ya wananchi walilielezea tukio hilo kuwa ni hujuma
inayofanywa na watumishi wasiojiamini kutokana na uchakachuaji wa vyeti na vielelezo
vingine vinavyowahusu ili kukwepa mkono wa sheria.
0 comments:
Post a Comment