Alfred
Mwanafunzi wa kwanza kitaifa, Alfred amesema
siri ya ufaulu wake ni kusoma kwa bidii na kumtegemea Mungu huku akieleza kuwa
alikuwa anatarajia kufaulu kutokana na jitihada alizokuwa nazo.
Alisema wakati akipigiwa simu kupewa
taarifa hizo, alikuwa kwenye mafunzo ya udereva Mwenge alipoitwa kwa simu
kutoka kwa Sekretari akamwambia mkufunzi wake amrudishe.
“Niliambiwa kuwa mama ananisubiri,
nilipokwenda akaniambia nimeongoza matokeo ya kidato cha nne, sikuamini nililia
kidogo lakini nikahisi kwamba mama ananitania, lakini ghafla akaniambia naitwa
shuleni hivyo tukaanza safari,”alisema.
Alisema alipofika shuleni alishangaa
wanafunzi wenzake wakiwa nje ambao walimwita huku na kule na kumpongeza lakini bado
akawa hana imani hadi alipoitwa na vyombo vya habari kuhojiwa, ndipo akaamini
kidogo.
“Yaani hadi sasa naona kama ndoto,
sijaamini bado kama nimeongoza sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu na
kuwasisitizia wanafunzi wengine kuhakikisha wanaishi katika ndoto ili waweze
kuzitimiza,” alisema.
Mama
Mama wa Alfred, Adela Shauri ambaye ni
mwalimu wa darasa la sita katika shule ya Msingi Mlimani alisema akiwa kazini
alipigiwa simu na walimu wa shule aliyosoma Alfred, kumtaka aende shuleni hapo.
Alisema baada ya kuambiwa hivyo
aliulizwa kuna nini, ndipo walipomweleza kuwa mwanawe ameongoza kitaifa kwenye
matokeo hayo na kwamba baada ya kusikia hivyo alifurahi sana hali
iliyochanganyika na kutetemeka.
“Ghafla nilitoka haraka nikaaga kwa
Mwalimu Mkuu kwamba nimeitwa shuleni kwa Alfred nimepata dharura, hivyo
nikachomoka nikaondoka kwenda kumfuata mwanangu chuo cha magari pale Mlimani,” alisema.
“Baada ya kumchukua Alfred nilimpigia
baba yake ambaye anafanya kazi ya Uhandisi kwenye Halmashauri ya Bagamoyo
akanieleza kuwa yuko kikaoni hivyo nimpigie baadaye lakini hadi muda huu hajui
na hana taarifa, hivyo atakaponipigia nitamwambia,” alisema.
Akizungumzia siri ya ushindi wa mtoto
wake, Mama Alfred alisema mwanafunzi huyo alikuwa anajisomea sana akitoka
shuleni licha ya kuhudhuria vipindi na masomo ya ziada na alikuwa na ratiba
zake binafsi.
Alisema Alfred alisoma shule za kawaida
akiwa msingi na kwamba darasa la kwanza hadi la pilli alisoma shule ya JK
Nyerere, Moshi, baadae Makongo hadi darasa la tano kisha shule ya msingi Mlimani.
Alisema shule ya sekondari alichaguliwa
kwenda Ilboru, lakini wakampeleka shule ya wavulana ya Feza ambapo alipata
punguzo la ada kwa asilimia 30 hali iliyosababisha unafuu kwa wazazi.
Mkurugenzi wa Feza, Ibrahim Yunus
alisema Alfred amekuwa mwanafunzi bora katika masuala mengi na amekuwa mshindi
wa kwanza kwenye uandishi wa insha na anatarajia kupewa tuzo mwezi huu.
Cynthia
Msichana wa pili kitaifa na aliyeshika
nafasi ya kwanza kwa watahiniwa wa kike kitaifa, Cynthia Mchechu alisema ana ndoto
ya kuwa mwanasheria.
Alisema ndoto ya kuwa mwanasheria
aliianza mwaka 2009 wakati aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye
aliapishwa mwaka huo akisoma baadhi ya vielelezo vyake kwenye mitandao ya
kijamii.
“Ndoto yangu ya kuwa mwanasheria inamhusisha
Obama kwa kuwa mwaka aliokuwa anaapishwa 2009 niliona vielelezo vyake vya
uanasheria hivyo nataka kuwa kama yeye na naamini ndoto hiyo itatimia,” alisema.
Alisema wakati anapigiwa simu alikuwa
ofisini shuleni kwao ambapo simu yake ilikuwa katika mlio wa kimya lakini mama
yake akampigia simu ya mezani ili apewe taarifa.
“Kwa kweli nilipoambiwa siwezi kusema
nilivyojisikia zaidi ya kulia kwa sikuamini kwa kuwa ni kitu ambacho kipo
lakini bado sijaamini na sijakubali, lakini naamini haya yametokana na mimi
kujisomea zaidi ya alichonifundisha mwalimu,” alisema.
Mama
Mercy Mchechu ambaye ni mama wa Cynthia
alisema mtoto wake amekuwa akifanya vizuri siku zote na kwamba amekuwa mtu
ambaye hufanya na husema vitu anavyoamini.
0 comments:
Post a Comment