Mwandishi Wetu
Shekhe Farid Had Ahmed |
MWENYEKITI wa Jumuia ya Maimamu Zanzibar
(Uamsho) Shekhe Farid Had Ahmed (45) na wenzake wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi
wamepeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ili Mahakama
hiyo imwite Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga aeleze upelelezi
umefika wapi, kwa sababu ni miaka mitatu bado wanapeleleza.
Maombi hayo yalipelekwa mahakamani hapo
kupitia mawakili watano wa washitakiwa hao, Abdubakari Salimu, Juma Nassoro,
Obed Hamidu, Daimu Halfani na Abdul Fataa, kutokana na upelelezi kuchukua muda
mrefu.
Mawakili hao wanataka kujua nini
kinakwamisha upelelezi wa kesi hiyo, kwa sababu makosa yanayowakabili
yanafahamika, kutokana na kwamba baadhi ya mashitaka hayo ni washitakiwa kuingiza
watu nchini.
Pia hati yao ya maombi inaeleza kuwa
kama wameshindwa kufanya upelelezi kwa kuona kuwa hapana ushahidi wowote wawaache
huru.
Mbali na Shekhe Ahmed, mshitakiwa mwingine
ni fundi ujenzi Jamal Swalehe.
Awali, Wakili wa Serikali, George Balasa
alidai kuwa wanakabiliwa na mashitaka manne, ambapo Shekhe Ahmed anakabiliwa na
mashitaka manne na Swalehe mawili.
Balasa alidai kuwa katika tarehe tofauti
kati ya Januari 2013 na Juni 2014, nchini walikula njama ya kutenda kosa
kinyume na sheria ya ugaidi.
Ilidaiwa Shekhe Ahmed na Swalehe
walipanga njama ya kuingiza watu nchini ili kushiriki vitendo vya kigaidi.
Mahitaka ya wanatuhumiwa kati ya Januari
2013 na Juni 2014, katika sehemu tofauti nchini walikubali kuingiza watu ili
kutenda vitendo vya kigaidi.
Katika mashitaka ya tatu dhidi ya Shekhe
Ahmed peke yake, akijua ni kinyume cha sharia, alimwingiza nchini Sadick
Absaloum na Farah Omary kushiriki vitendo vya kigaidi.
Wakili huyo, alidai pia katika mashitaka
ya nne dhidi ya Shekhe Ahmed peke yake, anatuhumiwa kutoa msaada wa kutenda
makosa ya kigaidi.
Washitakiwa hawakutakiwa kujibu
chochote. Mbali na washitakiwa hao kuna wengine zaidi ya 10.
0 comments:
Post a Comment