Ahmed Makongo, Bunda
LICHA ya kukumbana na ukatili wa kijinsia kama makundi
mengine ya kijamii, wanaume wametajwa kuona aibu kusema ukweli wanapofanyiwa
ukatili huo na wake zao.
Hayo yameelezwa jana na wadau mbalimbali walioshiriki
kikao cha majadiliano kuhusu ukatili wa kijinsia kilichoendeshwa na shirika
lisilokuwa la kiserikali la Zinduka, lenye makao yake makuu katika Mji mdogo wa
Nyamuswa wilayani Bunda kwa ufadhili wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation
For Civil Society.
Wadau hao wapatao 60 ambao ni wazee maarufu, wazee wa
mila, viongozi wa madhehebu ya dini, vyama vya siasa, watendaji wa vijiji na
kata, maafisa tarafa, pamoja na waandishi wa habari, walisema kuwa vitendo vya
ukatili wa kijinsi katika Wilaya ya Bunda, vimekuwa vikifanyika mara kwa mara.
Walisema kuwa licha ya vitendo hivyo kuonekana kwamba
vinawakumba watoto na wanawake, kundi jingine ni la wanaume ambao hufanyiwa
ukatili na wake.
Walisema kuwa baadhi ya wanawake wenye kipato kizuri
kuzidi waume wao wamekuwa wakiwafanyia ukatili wa kijinsia wanaume hao na
kufanya mwanaume husika kuishi kama watumwa.
“Vitendo vingine vya ukatili pia vinawakumba sana wanaume
hasa pale mwanamke anapokuwa ni kipato kuzidi cha mwanaume, hususan wale ambao
wamestaafu wamekuwa wakinyanyashwa sana na wake zao” alisema Sospeter Chacha
mzee wa kimila kutoka kata ya Guta
Hata hivyo, walisema kuwa elimu waliyoipata katika ki kao hicho wataifikisha kwa jamii
naowazunguka ili waweze kupata uelewa na kuoesha itendo ivo kiwa I pamja na
kuviba pindi vinapjitokeza.
“Tunalipongeza hili shirika la Zinduka kwa kuleta mradi
huu na mambo yote tuliyoyapata katika kikao hiki cha leo tutayapeleka kwa
wenzetu katika maeneo yetu ili kwa pamoja tuweze kupambana na vitendo hivi vya
ukatili wa kijinsia” alisema Anipher Maregesimama wa kimila kutoka kata ya
Neruma
Hata hivyo walisema kuwa ipo haja ya shirika hilo la
Zindka ambalo liko mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukaili wa kijinsi katika
jamii yetu kuendelea kutoa elimu kwa jamii, ili iweze kuachana na vitendo
hivyo ambavyo ni chanzo kikubwa cha kudhorotesha maendeleo, kiwa ni pamoja na
kuhamasisha wanaume kutokuwa wa kimya na kusema ukweli pindi wanapafanyiwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la
Zinduka, Maximillian Madoro, alisema kuwa kikao hicho ni cha majadiliano ili
kuona umuhimu wa namna yake na kuchukuwa hatua madhubuti za kukomesha na
kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba vikao hivyo ni endelevu
ikiwa ni pamoja na kusirikisha makundi mbalimbali ya kijamii.
Madoro alisema kuwa mradi huo ambao unagharimu kiasi cha
shilingi milioni hamsini utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita na unafanyika
katika kata 13 kutoka katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Bunda.
Alisema kuwa mradi huo utashirikisha wadau mbalimbali
wanapingavitend ivyo vya kaili wa ijinsia wakiwemo polisi, mahakama, wauguzi,
viongozi wa kisiasa, madhehebu ya dini, viongozi wa vijiji, maafisa watendaji
wa kata, maafisa tarafa, watendaji mbalimbali wa serikali na waandishi wa
habari.
“Mradi huu umefadhiliwa na shirika lisilokuwa la
kiserikali la Foundation For Civil Society (FES), kwa kipindi cha miezi sita na
utagharimu kiasi cha shilingi milioni hamsini na utashirkisha wadau mbalimbali”
alisema.
Mapema akifungua kikao hicho mkuu wa Wilaya ya Bunda
Lydia Bupilipili, pamoja na kulishukuru shirika hilo la Zinduka kwa kuleta
mradi huo, pia amliwataka wanajamii wilayani hapa, kuibua ukatili wa kijinsia
katika maeneo yao ili vitendo hivyo viweze kukomeshwa katika jamii yetu.
Aidha, aliwataka wanaume kutokuwa wakimya pindi
wanapofanyiwa vitendo ya kikatili na wake zao huku akisistiza kuwa
wanaponyamaza wakati wanafanyiwa vitendo hivyo ni sawa na kabali hali hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Ldyia
Bupilipili alisema kuwa atashirikiana na shirika hilo katika kuleta maendeleo
katika Halmashauri hiyo, ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa
kijinsia kwenye jamii.
0 comments:
Post a Comment