Sharifa Marira
Dk. Hussein Mwinyi |
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi, ametaka vijana wote waliosailiwa Juni kujiunga
na JKT kwa kujitolea, waripoti kwenye kambi walizopangiwa ifikapo Desemba mosi kwa kujilipia
nauli.
Ili kufanikisha suala hilo, Wizara imemtaka Mkuu wa JKT kufufua kambi ya Makuyuni,
ili iwe miongoni mwa zitakazotoa mafunzo kwa vijana wa JKT kabla ya Desemba mosi.
‘’Tunaomba Mkuu huyo pia ahakikishe shughuli
zote zinazofanyika hapo kambini kama vile shule, kilimo na ufugaji ziondolewe
mara moja, kambi ya Luwa na Milundikwa mkoani Rukwa, zirejeshwe kwa shughuli za
JKT za kilimo na ufugaji,’’ alisema Dk Mwinyi.
Aliagiza pia kambi ya Mpwapwa irejeshwe
kuendesha mafunzo ya kilimo na ufugaji ndani ya JKT, na kwamba utekelezaji wa
maagizo hayo unaanza mara moja na Mkuu wa JKT atatoa maelekezo ya utekelezaji
wake.
Alisema Juni vijana 14,000 waliohitimu
kidato cha sita walijiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, kumaliza
mkataba wao wa miezi mitatu Septemba.
“Serikali inataka vijana wote
waliomaliza kidato cha sita Mei ambao hawajajiunga na vyuo vya elimu ya juu,
wakaripoti kwenye kambi za JKT kwa utaratibu ambao Mkuu wa JKT ataelekeza,’’ alisema
Dk Mwinyi.
0 comments:
Post a Comment