Jemah Makamba
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Dar es
Salaam, imemhukumu kifungo cha maisha jela Hassan Athumani mkazi wa Kiwalani baada
ya mkukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka tisa.
Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi,
Juma Hassan alisema ushahidi uliotolewa dhidi ya mshitakiwa na shahidi namba
moja ambaye ni mtoto husika, unatosha kumtia hatiani Athumani.
Kwa mujibu wa Hakimu, mtoto huyo aliiambia
Mahakama kwamba mshitakiwa ni baba yake mdogo na alikuja kwao kutoka Tanga na
alikuwa akilala naye kitanda kimoja na ndipo alipomfanyia vitendo kinyume cha
maumbile.
Alidai wakiwa kitandani usiku, mshitakiwa
alikuwa akimwingiza uume wake, kisha kumtishia asiseme na akifanya hivyo
atampiga jambo ambalo lilimwogofya na alimfanyia hivyo kwa miezi mitatu.
Baada ya miezi mitatu motto huyo alipata
matatzo ya kutoka choo sehemu ya haja kubwa na kuamua kumwambia babu yake
kutokana na baba yake muda mwingi kuwa kazini wakati mwingine usiku kutokana na
kazi yake ya ulinzi.
Kutokana na hali hiyo walimpeleka
hospitalini kwa vipimo ili wapate uhakika kama kweli mtoto aliingiliwa na mshitakiwa.
Shahidi wa pili, Daktari Jamila wa hospitali
ya Amana alithibitisha mtoto huyo kuingiliwa kinyume na maumbile ingawa
hakukuonesha michubuko kutokana na mshitakiwa kumfanyia hivyo kwa muda mrefu.
Awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda
kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria cha
154(1)(a) na (2) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo alimlawiti
kwa miezi mitatu kuanzia Septemba hadi Desemba mwaka jana.
Mwendesha Mashitaka, Grace Mwanga
alisema hakuna kumbukumbu za nyuma za mshitakiwa, hivyo apewe adhabu kali ili liwe
fundisho kwa mshitakiwa na wengine wenye tabia kama zake.
Hakimu Hassan alimwambia mshitakiwa kama
ana chochote cha kuiambia Mahakama kabla hajatoa adhabu, mshitakiwa aliomba
asamehewe kwa kuwa ni mambo ya kibinadamu na aliyemshitaki ni kaka yake kabisa.
Hakimu hakuona kama hilo ni la msingi
hivyo akamhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela.
0 comments:
Post a Comment