Richard Mwangulube
MLIPUKO wa ugonjwa
wa Kimeta (Anthrax) umevikumba baadhi ya vijiji vya Wilaya Monduli mkoani
Arusha na kuua wanyamapori na mifugo ipatayo 140 hadi sasa.
Aidha, Serikali
imepiga marufuku ulaji wa wanyama waliokufa wenyewe na kutaka nyama
zinazopatikana kwa njia sahihi kupikwa vizuri ili kuepuka ugonjwa huo.
Ofisa Mifugo wa
Wilaya ya Monduli, Omar Sembe amesema ugonjwa huo uliozuka katika Kijiji
cha Selela hadi sasa umeua nyumbu 87, mbuzi
26, ngombe 12, swala 12 na kondoo 12.
Kwa mujibu wa
Sembe, mbali na ugonjwa huo kuua wanyamapori na mifugo, pia ni hatari kwa
binadamu hivyo kuna umuhimu wa kuongeza nguvu katika kuukabili.
Novemba 11, Halmashauri
ya Monduli Idara ya Mifugo ililazimika kuchukua sambuli za mizoga ya wanyama
waliokufa na kupeleka katika Kituo cha Kanda cha Uchunguzi wa Magonjwa ya
Mifugo (VIC), Arusha ili kujua chanzo chake na baadaye ilibainika kuwa walikufa
kwa kimeta.
Akizungumza
baada ya kutembelea baadhi ya vijiji katika eneo la Selela, Mkuu wa Wilaya ya
Monduli, Iddi Kimanta amepiga marufuku ulaji wa mizoga ya wanyama
waliokufa wenyewe
Kimanta ameagiza
kupalekwa haraka wataalamu wa mifugo na afya ambao watashirikiana na wafanyakazi
kutoka Shirika la Tanapa kwenda kufanyia uchunguzi suala hilo.
Mkuu huyo wa
Wilaya ya Monduli pia amesisitiza kuwa kufuatia mlipuko huo wilaya inatarajia
kuendesha kampeni katika vijiji vyote wilayani humo ili kuchanja mifugo yote
katika kampeni inayotarajiwa kuendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na
sekta binafsi.
Pia, ametaka mizoga
yote ya wanyamapori na mifugo kuzikwa ama kuchomwa moto ili kuepuka wananchi kuila.
Kutokana na
kuwepo na mwingiliano mkubwa wanyamapori na mifugo katika eneo hilo ndicho
chanzo kikubwa cha kuzuka kwa kimeta katika ukanda huo wa wilaya ya
Monduli.
Mkoa waArusha
una ngombe wapatao milioni 1,712,514, wa asili , ngombe wa
maziwa 198,330,mbuzi milioni 2,043,201 n kondoo
wapatao milioni 1,848,028.Ameeleza Chitukuro
0 comments:
Post a Comment