Dk. Sengondo Mvung |
WASHITAKIWA kumi wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi wameiomba Mahakama
iwaachie huru, baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa jalada la kesi yao lipo
kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) likisubiri uamuzi.
Mmoja wa washitakiwa hao, Masunga Makenza (40) alimuomba
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba aawaachie huru,
baada ya wakili wa Serikali Patrick Mwita kuieleza Mahakama hiyo kuwa jalada la
kesi yao awali lilikuwa kwa RCO na sasa lipo kwa DCI.
“Tunaomba leo hii tuachiwe , tuondoke tuende mtaani ,
kufuatia kauli ya rais ya hapa kazi tu. Kwa kazi hii ya upande wa mashitaka
tutafika? Wakikamilisha upelelezi watatukamata tena huko mtaani,” alidai
mshitakiwa huyo.
Mshtakiwa mwingine, Longishu Losingo aliomba upelelezi wa
kesi yao ukamilishwe haraka ili waondokane na mateso anayodai wanayapata
gerezani.
Aliiomba hati ya kifo cha mwenzao Chibago Magozi ipatikane
ili wasipate usumbufu baadaye. Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba
21, 2016 kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi
ambaye kwa sasa ni marehemu, John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Longishu Losingo
(29), Masunga Makenza (40), Paulo Mdonondo (30) , Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese
(33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30) .
Awali , akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Aida
Kisumo alidai kuwa washtakiwa hao Novemba 3, mwaka 2013 wakiwa eneo la Msakuzi
Kibwegere lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni, kwa pamoja walimuua Dk Mvungi.
0 comments:
Post a Comment